SIRI ILIYO WEKWA NA MUNGU NDANI YA UJANA

⛪⛪Somo: SIRI Iliyowekwa na MUNGU ndani ya Ujana wako👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

Maombolezo:3;27

✍🏾✍🏾Kijana kwa Hapa Tanzania katika sheria au utaratibu WA kumtabua katika katiba inasema  kijana Anaanzia miaka 18 mpaka 49 Miaka 50 huyu ni MZEE mpaka 100

Kijana inamtambua sheria kuwa ndio mwenye nguvu ya Kuifanya nchi yetu isonge mbele kimaendeleo na kukua kiuchumi nk

Ni kijana inamuelezea na kumpa umhimu na sifa zake

Lakini inamtaja kuwa ndio nguvu kazi ya Taifa LA Tanzania

Kwa hiyo ili ujana wake uwe na faida lazima Afanye mambo matatu katika nchi Yake

1⃣-Ajishughulishe kwa njia halali tena kwa jasho lake anapojishughulisha  Anaingiza kipato kwenye mfuko WA Taifa.

Hali itakayoifanya nchi Kupiga hatua ya kiuchumi.

2⃣-Atii na kufata mamlaka au Utaratibu WA nchi Yake pasipo kuvunja sheria za nchi.

Hali itakayomfanya awe mzalendo na Nchi Yake
Na mamlaka kumtambua uwepo wake kama RAIA mwema

3⃣-Aamini Na kuabudu popote Imladi kile kinachompa Aamini Hakivunji mamlaka yalipo au katiba ya nchi yetu.

Haya nimeeleza kadiri Roho Mtakatifu alivyonipa elimu kupitia Faida ya kijana kwa nchi Yake na SIRI Yake wajibu wake katika nchi Yake

⛪⛪Haya ni katika hapa duniani

Hayapishani sana na Mpangilio uliowekewa Na Baba kule mbinguni unayotakiwa uyafanye kabla ujafa.

⛪✍🏾Kwanza Tabua serikali ya mbinguni inamtambua kijana kama ndiye mwenye nguvu ndiye Anayeweza kuwakusanya wote wanaopotea ndiye mwenye injili ya moto Mwenye nguvu yakuihubiri injili kushuhudia kumsifu MUNGU Kumtumikia.

Kule mbiguni MUNGU Baba na Katiba ya mbiguni inamtambua kijana kwa mambo matatu Nayo akiyafata hayo Atakuwa MTU mwema na mzalendo kwake MUNGU Baba.

👉🏼1⃣-Kijana Anatambulika ndiye mwenye nguvu ya kuujenga ufalme WA MUNGU hapa duniani

Katiba inamweleza Yeye ni nguvu kazi WA mbiguni yeye ni mtafutaji yeye ni mwaminifu mbele za MUNGU.

Kwa hayo Yote Katiba ya mbiguni ikamuagiza Ajenge nyumba ya Bwana

2⃣-Ajitie Ujasiri na uhodari katika Yale Yampayo MUNGU sifa zake Asivunje sheria
Kwa tamaa za ujana haraka ya maisha aanze kutoa kafara watu au kwenda kwa waganga nk

Akienda hivyo Atakuwa Anavunja sheria na wale malaika Asikari Atazikusanya Data zote si kusema atakushika huwa ndio askari huyu Anakufatilia kwa ukaribu naye Huwa Anaweza kukutia pingu kukufunga gerezani

Hapo ndio kijana mipango huharibika mambo kuyumba nk

Ukijua ukaamua kurudi askari huyu huku achia

Hapendi uchochee ugomvi au umjaribu MUNGU ukiamua kufata   
Mfate na usivunje katiba ya mbinguni

3⃣-kijana Amepewa sifa ya kupambana na kuitetea Imani ya Yesu kristo mnazareth kwa nguvu zote kufa na kupona kwa ajili ya Yesu mnazareth

Awe kijana Anayeweza kupambana

Vita ya kimwili na kiroho kwa yeyote Anayetaka kuingia kupinga Vita au kuharibu injili

Asimame kwa maombi tu maana vita vyake vipi zidi ya

Majeshi ya shetani
Wapinga kristo
Wakuu wa dunia na Anga lake
Mungu ya Bahari

Kijana inamtambulisha atapingana vita na atashinda kwakuwa Anatetea Imani ya Yesu mnazareth Imani ya MUNGU.

Haya ni mambo Matatu yaliyopo mbiguni kisheria na katiba ya mbiguni imeyaeleza Soma

Kwenye katiba

Yoshua.1;3-9

Yeremia.1;5-10

2wakoritho.10;3-6

Ukipitia ibara hizi na mafungu haya kwenye Katiba ya mbiguni utaelewa kijana ilivyompa nguvu ya kupambana

⛪⛪mafundisho ya wajibu WA vijana⛪⛪

Nimefundisha kama Roho alivyonieleza na kunifundisha nami nimenena si Mimi kama Mimi

Na elimu hii ni Mafundisho ya Roho Mtakatifu si ya kimwili au elimu ya duniani hapa

✍🏾✍🏾By Pastor Richard

Mch.kiongozi Holy spirit ministry Tanzania

MOROGORO shukia VETA DAKAWA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.