Somo;Tabia 7 za Malaika
SOMO: TABIA 7 ZA MALAIKA. KARIBU KATIKA SOMO HILI UJIFUNZE KITU KUHUSU Somo hili la Tabia Za Malaika. Naenda Kuongelea Tabia Walizonazo malaika kule mbinguni 1;Ni Watiifu. Malaika wanatabia ya utiifu hwana Neno hapana kwa Mungu au Viongozi wao kila kitu husema ndio wanachoamriwa kufanya. Tusome;Mathayo:6;10 Zaburi;103;20 2;Ni Wacha Mungu Sana. Yaani Malaika Kazi Yao Kubwa Kumcha Mungu Usiku na mchana muda wote hufanya hivyo mbinguni. Tusome;Nehemia;9;6 Filip;2;9-11 3;Ni Wenye Busara Sana. Malaika hufanya kila jambo kwa hekima busara na maarifa ya juu. 1Petro;1;12, 1wafalme;8;39 4.Ni Wanyenyekevu. Malaika Wanatabia Ya Kunyenyekea Hawachukii wala kununa wala kupigana 2Petro:2;11,Yuda.9 5.Ni Wenye Nguvu Sana. Malaika mmoja anauwezo wa kuua majeshi au malaika wa shetani 1000 Anauwezo wa kuua Taifa au nchi nzima malaika mmoja Tu. Wananguvu kuliko kawaida. Tusome 2wafalme;19;35,Ufunuo.18:1,21 6;Ni Watakatifu Hawana Dhambi ...