SOMO:ISHARA 23 ZA MWANAMKE ANAEKUPENDA
SOMO: ISHARA 23 ZItakazokujulisha MWANAMKE ANAKUPENDA KWA DHATI Nawakaribisha Katika Nakala hii na Elimu hii ya ndoa kwa ajili yako Wewe uliyepo kwenye ndoa au Unaejiadaa Kuingia Mimi nayekuletea Nakala hii Naitwa Mwalimu wa Wanandoa TUSOME Mithali;9;9 Mithali;12;1-7 1: Anaonyesha ishara za Wivu Mwanamke anayekupenda huonyeshwa ishara za wivu. Hapendi kukuona ukiongea na mwanamke yeyote. Wakati mwingine huenda akasirika hata ukiongea na msichana wa familia yako. Wakati mwingine hudhania labda unayeongea naye mko na uhusiano wa kimapenzi. 2. Hukuangalia machoni bila kuogopa Ishara ya kwanza kabisa ni wakati mnapoangaliana macho kwa macho. Anapokuangalia machoni anaonyesha kuwa anakuamini na haogopi kuwa kwenye uhusiano na wewe. 3. Huonekana na wasiwasi anapokuona Hii hujitokeza sana kwa wanawake wengi. Mnapokutana, anaonekana kutaka ...