HAYA NDIYO YANAKUJULISHA MAHUSIANO YENU YANAENDA KUVUNJIKA
HAYA NDIYO YANAKUJULISHA MAHUSIANO YENU YANAENDA KUVUNJIKA Mithali:12;1-2 Mwalimu Wa Wanandoa @2021 Pastor Richard Najua wengi huwa hatujui Viashiria na Dalili zinazojulisha mahusiano yanaenda KUVUNJIKA Ukiyaona haya ujue uchumba unaenda kuvunjika 1;MAWASILIANO KUWA DUNI Kama mawasiliano yalikuwa ni mara nyingi kama tano kwa siku (kwa wale walio mbali.), na ukiona yanaaza kushuka hadi mara mbili hadi mwisho wa siku mawasiliano kukata kabisa. Na kila mmoja akiulizwa swali kwanini anasema nilibanwa na kazi basi hii ni hatua mbaya sana na hii huwa na athari sana pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi mwingine. 2:HASIRA ZA MARA KWA MARA. Hatua hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye kwake ni baya. Utajiongelesha ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo watu huwa wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake amamsaliti. 3:KUZUNGUMZA MANENO YASIYOFAA MUWAPO PAMOJA Hii ni hatua ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Mpenzi wako hutamu...