Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 7, 2026

SOMO:USIMAMIZI WA FEDHA KI-MUNGU

SOMO: USIMAMIZI WA FEDHA KI-MUNGU. Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro WhatsApp +255710889892 ​1. Usimamizi ni nini? ​Usimamizi ni sanaa au uwezo wa kutunza, kuongoza, na kuendeleza rasilimali ambazo umekabidhiwa na mmiliki halali. Katika muktadha wa fedha, msimamizi ni mtu anayetambua kuwa fedha na mali zote ni mali ya Mungu, na yeye amepewa dhamana ya kuzitumia kwa busara kwa ajili ya mahitaji yake, familia, na kazi ya Mungu. ​ Mistari ya Biblia: ​ Zaburi 24:1:   "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake." ​ 1 Wakorintho 4:2:   "Hapo tena inayohitajika katika mawakili, ni mtu aonekane kuwa mwaminifu." ​2. Hatua Unazotakiwa Kuzipitia ​Ili kuwa na usimamizi bora, unapaswa kupita katika hatua hizi nne: ➖​ Elimu na Maarifa:✍🏾  Huwezi kusimamia kile usichokijua. Jifunze misingi ya uchumi na kanuni za Biblia kuhusu fedha.. ​➖ Kutathmini Hali Yako (Assessment):✍🏾  Jua una kiasi gani, unadaiwa kiasi gani, na unatumia kiasi gani kwa mwezi....