JITAMBUE MZALIWA WA NGAPI UMEBEBA NINI
SOMO: JITAMBUE WEWE MZALIWA WA NGAPI NA THAMANI.. Kila mtoto huwa anakitu ambacho Mungu Alimwandalia Toka Tumboni Mwa Mama Yake katika somo hili utaelewa talanta ulionayo toka utotoni. Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro KA RIBU Kumb 33:1-9, Mwanzo 49:3-7; 1Kor 2:10 Kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu Aliye Hai, ameumbwa na nguvu maalumu kutoka mbinguni, ambayo ni mtaji wake maalumu; kiroho, kijamii na kiuchumi. Mwanzo 49:3 Reubeni u mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na nguvu. 1. MZALIWA WA KWANZA KATIKA FAMILIA YOYOTE* i. Amebeba nguvu nyingi za familia. ii. Amebeba Baraka za aina mbalimbali za wadogo zake. iii. Amebeba nguvu ya upendo ndani ya familia. iv. Mzaliwa wa k1wanza ni lango, Zab 24:7-9, ambapo Baraka zote za familia kutoka mbinguni zinapitia kwake na kuwafikia wadogo zake wote. v. Amebeba ustawi wa familia kiroho na kimwili. 2:MT...