SOMO;Uchumi na Kijana
SOMO;Uchumi na Kijana Maana ya Uchumi, Uchumi huweza kuelezewa kama jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao, huhusisha uzalishaji, usambazi, na utumiaji wa bidhaa, ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa ajili ya huduma mbali mbali, uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, jumuiya, mkoa, taifa au Dunia kwa ujumla. Uchumi ndio hutafsiri uwezo wa kumudu mahitaji. Teknolojia pamoja na utandawazi Teknolojia, ni kukua kwa sayansi ya uzalishaji katika Nyanja mbali mbali ka ma vile, kiuchumi, kisiasa, na kijamii, na utandawazi ni uongezekaji na muunganiko wa kiutendaji katika Nyanja mbali mbali kama vile kisiasa, kijamii, na kiuchumi, mara nyingi teknolojia ndiyo huzaa na kuieneza utandawazi. 2. MATABAKA YA KIUCHUMI DUNIANI Ni ukweli uliodhahiri kuwa utofauti wa kiuchumi katika nchi zetu, ndio unaopelekea hata uchumi wa watu wake wanaoishi humo, Kutokana na utofauti wa uchumi na mafanikio ya nchi zilizopo duniani, Dunia imejikuta katika matabaka ambayo ya...