SOMO :HIZI NDIO NJIA UTAMJUA MWANAUME TAPELI WA MPENZI MHARIBIFU
SOMO: HIZI NDIO NJIA ZA KUMJUA MWANAUME ATAKAYEKUOA USIPOPATA SIFA HIZI UJUE HAMUOANI Bwana YESU Asiwe watoto wa MUNGU Haya masomo nayaleta kwa Vijana wote wakae wajue na kuepuka kupitia katika4 Machungu YA kusalitiwa katika Mapenzi Kwa sababu vijana wengi siku hizi hutumia njia ya kusema kuowa wakiwa wanataka Bint wampate wazini nae tu kisha wamzalishe au kumharibia malengo yake na mipango. Binti Yangu nimekuletea Somo hili Ambaye hujaolewa Ujue sifa ya mwanaume muoaji Anakuaje Hii ikupe ufahamu. Usijirahisishe na kukubali kuitwa mama kabla ya kuitwa mke wa mtu. Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania nakuandalia nakala hii fupi yenye maarifa makubwa. Tunasoma Zaburi 119:9 Mithali 7:7 1.MWANAUME MWENYE LENGO LA KUKUOA ATAKUPA NAFASI YA KWANZA KWENYE MAISHA YAKE. Yaani ktk mahusiano ya uchumba tu utaanza kujiona queen. Wanaume waoaji tunafanya hivi ili ndege mzuri asirukie mti mwingine kwa hi...