Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 13, 2021

MWANAUME AMBAYE ASIYEFAA KUKUOA

Picha
MWANAUME AMBAYE ASIYEFAA  KUKUOA NI MWENYE SIFA HIZI 1. Mwanaume Kicheche: Hakuna mwanamke anayependa kuchezewa na wanaume, labda tu kama anafanya hivyo katika juhudi zake za kujikwamua kiuchumi, lakini pale mwanamke anapokuwa katika harakati za kutafuta mwanaume ambaye kama mambo yakiwa mazuri wafunge ndoa, ni vyema akajiepusha na wanaume vicheche wanaotongoza wanawake kwa lengo la kustarehe na kumaliza matamanio yao ya ngono. wakati mwingine mwanaume mwenye tabia ya kuchezea wanawake anaweza kumfuata mwanamke ambaye ametamani mwili wake na kujifanya eti amebadilika na kuwa mtakatifu. Anaweza kujiweka katika mazingira yanayoonyesha kwamba amebadilika ili kumvuta mwanamke. Shituka mwanamke, jasiri haachi asili atakutumia kama condom na kisha kukutupilia mbali. Wanaume wenye tabia hizo ni vigumu kubadilika. Inahitaji subira ya hali ya juu kujiridhisha kama kweli amebadilika au anazuga ili apate anachokitaka. 2. Mwanaume asiye na kazi na asiyejishughulisha: Mwaume asiye na kazi...