Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 26, 2026

SOMO: UTUNZAJI WA AKILI

SOMO: UTUNZAJI WA AFYA YA AKILI: "Akili Iliyofunguliwa kwa Ajili ya Utukufu wa Mungu" ​UTANGULIZI Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania ​Watu wengi makanisani wanadhani matatizo ya akili ni pepo pekee, lakini neno la Mungu linatufundisha kuwa akili ni sehemu ya ibada yetu ( Mathayo 22:37 ). Akili yenye afya ni ile inayoweza kufanya maamuzi sahihi, kukabiliana na mikazo ya maisha, na kufanya kazi kwa tija. ​1. ADUI WA AFYA YAKO YA AKILI ​Ili tulinde afya ya akili, lazima tujue nini kinaishambulia: ​ Hofu na Wasiwasi: Huvuruga uwezo wa kufikiri ( 2 Timotheo 1:7 ). ​ Msongo wa Mawazo (Stress): Kutokana na madeni, changamoto za kifamilia, au kazi. ​ Majeraha ya Kihisia: Uchungu, kutokusamehe, na kukataliwa. ​ Uchovu wa Mwili: Kukosa mapumziko kunadhoofisha mfumo wa fahamu. ​2. NGUZO TANO ZA KUIMARISHA AFYA YA AKILI ​Ili akili yako iwe na nguvu, unapaswa kuzingatia haya: ​ A. Kulisha Akili Neno la Mungu Akili yako i...