SOMO; UBATIZO WA MAJI MENGI
SOMO: UBATIZO WA MAJI MENGI WA KIBIBLIA Ni muhimu kufahamu kuwa Yohana mbatizaji alimbatiza Yesu katika maji tele (MATHAYO 3:13-17 ). Yesu Kristo alibatizwa katika mto Yordani kwasababu huko kulikuwa na maji tele. Yohana mbatizaji alikuwa akibatiza sehemu zenye maji tele ili watu waweze kuzamishwa katika maji kama tutakavyoona maana ya ubatizo na kwa nini kuzamisha katika maji tele. Yohana mbatizaji hakubatiza Yordani tu, alibatiza Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. YOHANA 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwasababu huko kulikuwa na maji tele, watu wakamwendea wakabatizwa”. Ubatizo lazima ufanye kwenye maji tele ya kumtosha mtu kuzamishwa. MAANA YA NENO KUBATIZWA A...