Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 19, 2025

SOMO:NIFANYE NINI NIFIKE MBINGUNI

SOMO: NIFANYE NINI NIFIKE MBINGUNI.  YEREMIA;10:13_17 Mwanzo: Sura ya 7 Na 8 Mwanzo:27:28, 39 Kumb. Torati:14:35 Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro Kanisa la Holy Spirit church Tanzania Morogoro Veta Dakawa Karibuni Watoto Wa Mungu Tu jifunze Tunafanyaje nini nifike Mbinguni au Tupate Kigali na Sisi Kwa Mungu Sababu hatuwezi kumfurahisha Mungu Endapo Swali ndogo kama hili Tutasema Tufanye mema tu ndiyo Tufike Mbinguni Lazima Tujue Kuna visababishi vyakutufanya Tufanye Vizuri Na Tupate kukubalika katika Mbingu.  Mbinguni ni Makao Ya Mungu Wetu hapa chini ni Sehemu ya kuwekea Miguu Yake.  Tunaposema "MUNGU" Ni Roho lakini  kazi zake anazifanya Kimwili na kiroho Mwanzo 1:2   Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. KUNA MAMBO HAYA YAFANYE ILI  UFIKE MBINGUNI 1;MPENDE MUNGU WAKO.  Vitabu:Kumb.Torati.6:5 Luka. 10:27 Kumpenda Mungu huhusisha maeneo Manne ya mwili wako...