SOMO:MAMBO YANAYOVUNJA NDOA
SHULE YA WANANDOA NA WANAOJIANDAA KUINGIA. SOMO: MAMBO YANAYOVUNJA NDOA NYINGI AU KUTOELEWANA KWA WANANDOA MWALIMU; PASTOR RICHARD Nipo; Morogoro Veta Dakawa Simu+255759861768 Kwa ushauri na msaada piga Jioni 12;00 Haya nayoenda kueleza unatakiwa uwe makini nayo ili kuifanya ndoa Yako iwe Bora na yakuingwa. Tusimame mithali;14;1, 2Yohana: 1 10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, 1: MARAFIKI,WACHUMBA,NA MAWASILIANO YA SIMU ZISIZO NA FAIDA. Vijana wengi wanaingia kwenye ndoa wanajua ndoa nikuvaa shera na suti hawajui Ni maisha mapya yanayoitaji ujenge Safu mpya sio marafiki uliokuwa nao kabla hujaolewa au Kuoa na uagalie Hata watu utakaoanzisha urafi nao. ✍️✍️UNASHAURIWA✍️✍️ Uwe na marafiki wenye hofu ya Mungu, Wanaozilea ndoa zao vizuri,Wenye ushauri mzuri wa Kiroho na kimwili. Badilisha laini zako na vunja laini ya zamani uaze mawasiliano na watu wapya Kabisa hakikisha Kama ulikuwa na wachumba au na mawasiliano ya Siri achana nayo. ...