MAOMBI YAKUJIONDOA KWENYE NGUVU ZA NGIZA AU UHARIBIFU
SOMO;NGUVU YA MAOMBI YAKUJIONDOA NA UHARIBIFU WA NGIZA Karibuni Katika Maombi Naitwa Mchungaji Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa @2020/8 Maombi haya ni kwa ajili ya wale ambao wanataka au wanatamani kujiondoa kwenye maagano ya Uharibifu, au maagano na nguvu za giza. Maagano ya Uharibifu yapo kwa ajili ya ya kuharibu tu na si vinginevyo, na kadiri yanavyoendelea kuwepo Uharibifu hauepukiki. Maagano yanayozungumziwa hapa ni yale ya kurithi au yaliyoingiwa na mhusika aidha kwa kujua au pasipo kujua kama anaingia kwenye maagano. Kwa sababu ni maagano ya uharibifu ni muhimu kujiondoa au kuvunja maagano hayo. Ili kuyavunja ni lazima utangaze kuyavunja, na inawezekana maagano mengine yapo hapo muda mrefu, kwa hiyo ni lazima kuomba kwa bidii soma Yakobo 5:16 Angalizo: Usiombe Maombi haya bila maelekezo,kama huelewi chochote Wakolosai 2:14-15, Wagalatia 3:13-14 Wakolosai 2:14-15, “akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akai...