JITAMBUE MZALIWA WA NGAPI UMEBEBA NINI

SOMO: JITAMBUE WEWE MZALIWA WA NGAPI NA THAMANI..


Kila mtoto huwa anakitu ambacho Mungu Alimwandalia Toka Tumboni  Mwa Mama Yake katika somo hili utaelewa talanta ulionayo toka utotoni.

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro 

                   KARIBU

Kumb 33:1-9, Mwanzo 49:3-7; 1Kor 2:10

Kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu Aliye Hai, ameumbwa na nguvu maalumu kutoka mbinguni, ambayo ni mtaji wake maalumu; kiroho, kijamii na kiuchumi.

Mwanzo 49:3
Reubeni u mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na nguvu.


1. MZALIWA WA KWANZA KATIKA FAMILIA YOYOTE*


i. Amebeba nguvu nyingi za familia.
ii. Amebeba Baraka za aina mbalimbali za wadogo zake.
iii. Amebeba nguvu ya upendo ndani ya familia.
iv. Mzaliwa wa k1wanza ni lango, Zab 24:7-9, ambapo Baraka zote za familia kutoka mbinguni zinapitia kwake na kuwafikia wadogo zake wote.
v. Amebeba ustawi wa familia kiroho na kimwili.

2:MTOTO WA PILI KATIKA FAMILIA YOYOTE*


i. Ni mbeba neno la uzima.


ii. Kipawa cha ualimu kinakaa vizuri sana ndani yake.


iii. Amepewa neno la uzima la kusaidia kanisa familia na nchi.


3. MTOTO WA TATU KATIKA FAMILIA YOYOTE


i. Ni mtawala katika ulimwengu wa roho na wa mwili.
ii. Ni mtunga sheria popote atakapokuwa anaishi, anasoma au anafanya kazi.
iii. Amepewa mamlaka ya kusimamia jamii, kuiongoza na kuitawala.
iv. Anafaa kuwa mwanasheria au kiongozi popote aendapo.


4. MTOTO WA NNE KATIKA FAMILIA YOYOTE


i. Amepewa neema ya kumiliki utajiri wa nchi.


ii. Kama akijitambua na kusimama katika zamu yake, ajue amepewa neema na nguvu ya kuutawala uchumi vizuri sana.


iii. Amepewa nguvu ya kumiliki utajiri wa mbingu na dunia.


*5. MTOTO WA TANO KATIKA FAMILIA YOYOTE*


i. Amepewa neema ya kushinda changamoto.
ii. Amepewa stamina ya kushindana na majaribu kwa asili.
iii. Amepewa neema ya kutumika na upako wa juu sana, kama akiokoka na kujitambua, na kusimama katika zamu yake.

6. MTOTO WA SITA KATIKA FAMILIA YOYOTE


Ni mtu wa ujuzi, na talanta. Na Amepewa nguvu ya ubunifu wa pekee.


7. MTOTO WA SABA KATIKA FAMILIA YOYOTE*


i. Amebeba uheri wa Mungu Mtakatifu.
ii. Yeye ni jubilee, yaani maachilio.
iii. Usithubutu kushindana naye maana hautafanikiwa.
iv. Ukimshitaki hauwezi kufanikiwa.
v. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.
vi. Anafaa kuwa hakimu kama ataamua kuichukua taaluma hii.
vii. Ukipata kesi yoyote na akakusindikiza ni lazima utashinda, maana utu wake wa ndani ameumbiwa neema hii.8

*8. MTOTO WA NANE KATIKA FAMILIA YOYOTE*


i. Amebeba nguvu ya utumishi.
ii. Amepewa neema ya kusaidia wengi kiuchumi, kiroho na kijamii, kama akijitambua na kusimama katika zamu yake.

iii. Akiokakoka na kuwa mtumishi kanisa lolote, atalisaidia sana kustawi, kwa kuwa ni mtu wa kutegemewa sana.
iv. Amepewa neema ya kuwa nguzo.
v. Ukimtambua katika kanisa lako na kumthamini, na kumtumia vizuri, utafanikiwa sana.

*9. MTOTO WA TISA KATIKA FAMILIA YOYOTE*


i. Ni m’beba karama.
ii. Akipokea kipawa anakitunza sana kwa muda mrefu.
iii. Amepewa nguvu ya umoja.
iv. Ni mtu anaweza kuinganisha jamii, nchi au familia na kuleta mshikamano.
v. Anafaa kuwa mwanasiasa endapo akijitambua na kusimama katika nafasi yake aliyokirimiwa na mungu.

*10. MTOTO WA KUMI KATIKA FAMILIA YOYOTE*


i. Yeye ni msamaha.
ii. Amekirimiwa nguvu ya msamaha.
iii. Amepewa uwezo wa kusuluhisha migogoro kwa ufanisi wa hali ya juu sana.
iv. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.

*11. MTOTO WA KUMI NA MOJA KATIKA FAMILIA YOYOTE*

Ni faraja kwa familia.
Kuna wakati anapata tatizo la kukataliwa, lakini ni mvumilivu sana.
Mkikaa naye kwa upendo mtabarikiwa sana.


  • Mifano ya wazaliwa wa kwanza.

A. WAZALIWA WA KWANZA KIMWILI 

  1. Kaini mzaliwa wa kwanza kwa Abili (Mwanzo 4:1-2)
  2. Yafethi mzaliwa wa kwanza kwa ndugu zake Shemu na Hamu ( Mwanzo 10:21)
  3. Nahori mzaliwa wa kwanza kwa ndugu zake wawili Abramu / Ibrahimu na Harani.
  4. Ishmaeli mzaliwa wa kwanza kwa Isaka
  5. Esau mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo. N. K

B. WAZALIWA WA KWANZA KIROHO;

  1. Habili mzaliwa wa kwanza kwa Kaini ( Waebrania 11:4)
  2. Shemu mzaliwa wa kwanza kwa ndugu zake ( Mwanzo 5:32)
  3. Abramu / Ibrahimu mzaliwa wa kwanza kwa ndugu zake Nahori na Harani ( Mwanzo 11:26)
  4. Isaka mzaliwa wa kwanza kwa Ishmaeli ( Ndiye aliyekuwa mtoto wa agano Mwanzo 17:21)
  5. Yakobo mzaliwa wa kwanza kwa Esau ( Mwanzo 25:23)
  • Yesu Kristo ndiye ndugu mkubwa na mzaliwa wa kwanza kwa wote, maana katika Yeye utimilifu wote wakaa ( Wakolosai 1:18)


                 By Pastor Richard
Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.