SOMO; NGUVU YA UMILIKI WA UKOO
SOMO: NGUVU YA UMILIKI KATIKA UKOO Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro Katika Familia au ukoo huwa Lazima Uwe na Nguvu ya kumiliki. Mfano: Elimu madaraka Imani na Pesa Familia Yoyote Lazima Awepo Mtu mwenye cheo kama familia Ya Yese Au Ibrahimu nk Neno Kuu: “Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; na mali ya mwenye dhambi huwekewa mwenye haki.” (Mithali 13:22) 1. Msingi wa Umiliki: Agizo la Kiungu Mungu ndiye aliyeanzisha mfumo wa koo na familia, na alikusudia kila ukoo uwe na sehemu yake ya kumiliki ili kujiendesha. Andiko: Mwanzo 1:28 "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha..." Tafakari: Kuitiisha nchi maana yake ni kuitawala na kuimiliki. Ukoo usioiliki rasilimali hauwezi "kuitiisha" nchi, badala yake unatiishwa na kutaabika. 2. Umiliki wa Ardhi na Urithi wa Kudumu Katika Biblia, ardhi haikuwa mali ya mtu mmoja tu, bali ilikuwa ni dhamana kwa ajili ya ukoo mzima ili kuhakikisha hakuna kizazi kinachokuja ku...