Somo;ACHA TABIA INAYOKWAMISHA UPENDO NDANI
✍️✍️SOMO:JINSI YA KUIACHA TABIA INAYOMKWANZA MWEZI WAKO NDANI YA NYUMBA ✍️✍️ Umri Miaka 18 Wanaruhusiwa Masomo haya Mithali;14;1 Isaya;58;12 ✍️✍️ MASOMO YA WANANDOA ✍️✍️MWL: PASTOR RICHARD ✍️✍️NIPO Morogoro veta Dakawa ✍️✍️Simu +255759861768 Wanandoa Tuongee Tunakutana Tena katika DARASA la KuZijenga ndoa Zetu zilizobomoka Kupitia Tabia Zetu Wanandoa ndani Ya Nyumba. Kati ya kitu ambacho kinasumbua wengi na kimekwamisha wengi ni tabia.Wengi wana huzuni ndoa zimewashinda,kazi zimewashinda,fedha na mafanikio vimewakimbia,watoto wamewashinda,hawana marafiki hata miili yao haina afya kwa sababu ya tabia tu. Wengine wamejiona ni kama wana laana,wengine wanafikiri labda wanaugua ugonjwa flani lakini shida siyo shida nitabia zao tu. Hebu tuone namna gani tunaweza badilika au kubadilisha tabia zetu. ✍️✍️T...