Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 4, 2022

SOMO; Faida ya Hekima

       SOMO: FAIDA YA HEKIMA Hekima kwako inafaida Sana kuliko kitu chochote Unachoweza Kutenda Tengeneza maisha yako yapate nafasi kuipa hekima iamue.  1.  Itakuwezesha kujanga nyumba imara na kuwa na mahusiano imara ya kifamilia. Mithali 24:3   Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika. Mithali 19:13   Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke ni kama kutona-tona daima. 2.  Itakufanya upate kibali katika yale unayoyafanya. Mithali 14:35   Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu. Mithali 17:2  Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwama atendaye mambo ya aibu;.. 3.  Itakuwezesha na vikwazo na upinzani Mithali 21:22   Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu; Na kuziangusha nguvu za tumaini lao. Mithali 24:5  Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam mtu wa maarifa huongeza uwezo. Muhubiri 9:18a   Hekima ndio bora kuliko silaha...