Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 7, 2026

SOMO:KUMEZWA NA ADUI YAKO

SOMO: KUMEZWA NA ADUI YAKO ​Katika maisha ya kiroho na kijamii, "kumezwa" kunamaanisha hali ya kupoteza utambulisho wako, nguvu zako, au kusudi lako kwa Sababu ya Kuzidiwa na Changamoto na Kipindi Kisumu.  Jambo lolote linalokushikilia Lazima likutapike Kama Samaki alivyoshindwa Kumshikilia Yona. au Kaburi lilivyoshindwa Kumshikilia Yesu Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro. ​1. HASARA ZA KUMEZWA ​Kumezwa na adui kuna madhara makubwa yanayoweza kufuta kabisa hatima ya mtu: 1:​ Kupoteza Utambulisho na Sauti: Unapomezwa, sauti yako haisikiki tena na utambulisho wako unafutika ndani ya adui.   ​ Mstari:   1 Petro 5:8  –  "Mwe na kiasi, mkeshe; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka, akitafuta mtu ameze." 2:​ Kuzikwa kwa Malengo na Maono Yako.  Adui anapokumeza, anazuia nuru yako isionekane, na mipango yako inafia ndani ya tumbo la changamoto.   ​ Mstari:   Yeremia 51:34  –  "Nebukadreza mfalme wa Babeli ameni...