SOMO : MJAMZITO NA TENDO LA NDOA
*SOMO:MJAMZITO NA TENDO LA NDOA* Pastor Richard Darasa La Wanandoa Simu +255759861768 👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽 Wakati wa ujauzito wanawake wengi hukosa hamu ya tendo la ndoa hivyo mwanaume unahitaji kuwa na mawasiliano mazuri ili mambo yaende vizuri. *Je, Mwanamke mwenye mimba anaweza kuendelea na tendo la ndoa* ? Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba tendo la ndoa kwa mwanamke mwenye mimba ya hatua yoyote ya ujauzito inaweza kumuathiri mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni ( fetus) Hata kama kunatokea miscarriage bado sayansi inathibitisha kwamba chanzo huwa si sababu ya tendo la ndoa wakati mwanamke ana mimba, bali sababu zingine kabisa. Tafiti nyingi zimefanywa kwa kufuatilia wanawake ambao waliendelea na tendo la ndoa huku wakifika kileleni ( orgasm) na wale ambao hawakuwa wanafika kileleni wakati wa tendo la ndoa, na wale ambao hawakufanya kabisa tendo la ndoa muda wote wa ujauzito...