Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 6, 2026

SOMO: NDANI YA TU MBO LA SAMAKI

SOMO: NDANI YA TUMBO LA SAMAKI (Mtazamo wa Wanandoa) UTANGULIZI; Zipo ndoa Nyingi Zinaishi Ndani Ya Samaki Sehemu Ya Marekebisho Ya Changamoto Wanandoa Wengi Wakimbia Majukumu Yao Hali inayomfanya Adui azitese Ndoa Zao.  Yona:2 huu mkasa Tunaupata ​1. "Tumbo la Samaki" kama Sehemu ya Marekebisho ​Yona aliingia tumboni mwa samaki kwa sababu ya kukimbia wajibu wake. Katika ndoa, kuna wakati mmoja au wote wawili "wanakimbia" majukumu yao (upendo, uaminifu, au mawasiliano). ​ Changamoto:   Unapojikuta katika hali ya giza na msukosuko ndani ya nyumba, usitazame kama mwisho wa safari, bali tazama kama nafasi ambayo Mungu ameruhusu ili muweze kutulia na kutafakari mlipokosea njia. ​2. Maombi ya Pamoja Katika Giza ​Yona hakuwa na mahali pengine pa kwenda; alikuwa amebanwa pande zote. Wanandoa wanapopitia "tumbo la samaki" (kama vile changamoto za kiuchumi au kutokuelewana), ni wakati wa kuacha kunyoosheana vidole na kuanza kunyoosha mikono juu kwa Mungu. ...