SOMO; MBINU ZA KUVUNA WATU
SOMO: MBINU ZA KUVUNA WATU NA KUWALETA KWA YESU Karibuni SOMO hili Nzuri Kuvuna watu (Uinjilisti) si kazi ya wahubiri pekee, bali ni agizo la kila mwamini. Ili kufanikisha hili, tunahitaji mkakati wa kiroho na wa kiutendaji.Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Karibu. 1. Maandalizi ya Kiroho (Maombi ya Upatanisho) Kabla ya kusema na watu kuhusu Mungu, lazima useme na Mungu kuhusu hao watu. Maombi hulegeza mioyo migumu na kufungua milango ya ufahamu. Andiko la Kusoma:- : “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote.” (1 Timotheo 2:1) Mambo Ya Kufanya: 1:Omba Roho Mtakatifu akupe 2: "Macho ya Kiroho" kuwaona wenye uhitaji.. 3:Vunja ngome za shetani zinazowazui 4:Omba Mungu akukutanishe na mtu ambaye moyo wake umeshaandaliwa. 2. Jenga Uhusiano wa Upendo (Ushuhuda wa Maisha) Watu wengi huvutiwa na tabia yako kabla hawajavutiwa na maneno yako. Upendo ni lugha inayoeleweka na kila mtu. Andiko la Kusoma “Vivy...