MAOMBI YA UKOMBOZI KUTOKA KWENYE ROHO YA KUKATALIWA
MAOMBI YA UKOMBOZI KUTOKA KWENYE ROHO YA KUKATALIWA. Kukataliwa ni kukosa kibali kwa wanadamu kila unalofanya Wanakudharau na kukucheka saa nyigine Kukudhihaki. Ukiwa una roho hii utapata wachumba wanakukataa ukienda kuomba kazi napo wakupokelea documents lakini nafasi za kazi hakuna kama ni kijana mwanamke anakuwa hakupendi kila unayemtongoza hakukubali hii roho kwa ufupi ni mbaya.sana. Nayekuletea maombi haya Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Twende Tukaombe Wote MSTARI TUTAKAOSIMAMA NAO. 👇👇👇👇👇👇 1 Timotheo 4:4-5 [4]Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; [5]kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. HATUA ZA KUFATA MUONGOZO WA KUOMBA 1.ANZA NA TOBA Omba toba kila eneo ulilokosana na Mungu 2.MSHUKURU MUNGU Mwelezee uzuri wake mwambie umeniumba vizuri nafurahia uzuri ulionipa Bwana. MTIRIRIKO WA UOMBA...