Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 19, 2022

SOMO; MAFANIKIO KUPITIA PESA ZETU

S OMO;MAFANIKIO KUPITIA PESA ZETU KIBIBLIA Kutumia vyema fedha ambazo Mungu ametupa ni changamoto kubwa katika maisha. Kumbuka kuwa tutatoa hesabu ya vile ambavyo Mungu ameviweka mikononi mwetu. Ni jukumu letu kufanikisha maisha yetu kwa zile fedha ambazo Mungu ametupa, kila mkristo ni lazima ahakikishe anafanikiwa katika suala la uchumi kwa utukufu wa Mungu. Kuna mambo matatu inabidi tuelewe Fedha ni muhimu katika maisha yetu Mipango ya matumizi ya fedha ni muhimu kuliko fedha zenyewe Dhamira na nia yako ya kutumia vizuri fedha zako ni muhimu zaidi katika uwakili wako Sahihi  Mafanikio yanakuja unapokuwa na mtazamo sahihi 1.Jitoe kikamilifu kwa Mungu Mungu alimbariki Abraham kwa sababu alijitoa kikamilifu kwa Mungu, akaacha nchi  yake na kwenda kule Mungu alipomwambia aende bila kujua aendako.  Mwanzo 13:12-18. Ebrania 11:8-10    8Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende kwenye nchi ambayo Mungu angempa kama urithi. Naye aliondoka akaenda ingawa hakujua...