SOMO:NDOA

✍️✍️SOMO; NDOA

Mwanzo;2:20-24 Mithali;14;1-3 Mithali;7;7-10

✍️✍️DARASA LA WANANDOA
✍️✍️ MWALIMU WA WANANDOA
✍️✍️Nipo Morogoro Veta Dakawa

Habari za muda huu....ndugu jamaa na marafiki....bila shaka sote tu wazima na wa afya njema....wenye maradhi Mungu muweza awajaalie uzima.....na afya....

Bila ya shaka kila mmoja amekuwa akijiuliza swali hili na kila mmoja amekuwa na tafsiri yake kwa namna anavyoona yeye kwenye ulimwengu wake.......

NDOA tafsiri yake ni.....
Muunganiko wa nyoyo mbili zilizopendana kwa dhati....na kuamua kuishi pamoja katika kipindi chote cha maisha yao....wakilifurahia pendo lao......

Kwa maana hiyo NDOA ni tukio lenye furaha na kuishi ndani ya ndoa....ni jambo la furaha....na kutumia kipindi chote cha maisha yako...na yule ambaye ni chaguo la moyo wako....ni jambo la furaha na lenye kusisimua zaidi.....

Lakini vile vile kuishi na mtu hata kama nyoyo zenu zimeshibana...sio jambo rahisi na lina changamoto nyingi sana....hivyo basi lazima kuwe na nguzo imara za kuweza kuilinda NDOA yenu ili nyote mpate kuyafurahia maisha ya ndoa.......

Misingi ifuatayo ni nguzo imara zinazoweza kuifanya ndoa yenu idumu milele na huku kila mmoja akifurahia muunganiko huo......

✍️✍️NGUZO 5 ZA NDOA

>UPENDO....,
Huu ndio msingi mkuu....kwenye ndoa kwani msingi huu....huwa unakuja automatic na ndio chanzo kikuu kinachowakutanisha wana ndoa.....na hatimaye kufikia kuamua kuishi pamoja......kama mke na mume....

Kabla hujaamua kufunga NDOA na mtu.....jambo la kwanza ni wewe kutafuta sehemu tulivu ukiwa pekee yako....na kusema na nafsi yako.....huku ukipitia vipimo vyako vya mapenzi......hakika nafsi zetu haziongopi.....ila tu huwa tunaamua kuzidhulumu na kuzikatili kwa tamaa za vitu mbali mbali......
Sema na moyo wako na jibu utalipata.....

>KUVUMILIANA.....,
Ingawa tumeunganishwa na upendo wa dhati baina yenu.....lakini sisi kati yetu bado ni wanadamu....na kama ilivyo mwanadamu ni kiumbe dhaifu na kuna nyakati anatoka nje ya mstari.....ikiwa huna moyo wa uvumilivu....huwezi kuishi na mwanadamu hata kama unampenda kwa kiwango gani........

Hata wazee wetu tunaowaona wakimaliza miongo mingi ya kwenye ndoa si kwamba hakuna mkosefu kati yao....isipokuwa uvumilivu ndio umewafanya kufikia pale......

Hivyo kuvumiliana na nguzo muhimu sana kwenye kudumisha ndoa.....

> KUSAMEHE....
Kama ambavyo nimeelezea hapo juu kuwa sote si wakamilifu na kuna nyakati tunatoka nje ya mstari.......ingawa makosa mengine ni yenye kuchoma moyo kama sio kuumiza....lakini kuliweka jambo moyoni....ni mbaya zaidi kuliko hata ubaya wa jambo lenyewe......hivyo tunatakiwa kusamehe ili kuziponya nyoyo zetu......

Mwanafalsafa mmoja alipata kusema kuwa.....
"Kushikilia hasira mioyoni ni sawa na kushikilia kaa la moto...ambapo kabla halijamdhuru adui yako...kwanz linaanza kukuchoma wewe.....

Hivyo tunatakiwa tuache mambo yaende na kuendelea kuyafurahia maisha yaendelee......

>KUTHAMINIANA......
Kila mmoja wetu huwa anajisikia raha sana...pale anapojihisi kuthaminiwa......hata kama ulimwengu mzima utakutenga lakini mtu mmoja.....anayekuthamini na kukujali....kunaweza kukufanya wewe ujione wa kipekee hapa ulimwenguni......
Hivyo hivyo....hata kwenye NDOA kama mnathaminiana....kila mmoja anaona umuhimu wa mwenzie na kamwe hamuwezi kuchokana.....hivyo ndoa kudumu.....

>KUSHIRIKIANA......
Tangu mlipokula kiapo na kuamua kuishi pamoja.....maana yake nyie mmeshakuwa mwili mmoja.....kama ilivyo katika mwili kuwa msawazo wa utendaji kazi wa mwili ni kutokana na ushirikiana wa viungo na organi zote katika mwili.....
Hivyo basi jukumu la kutunza na kuilinda ndoa ni la kila mmoja wenu......kila mmoja kwa nafsi yake anapaswa kulipigania hilo....sio kumfanya mwenzio mtumwa kana kwamba amejioa mwenyewe.....
Hata wanafiki na wambeya hupata wakati mgumu kuwafitinisha wanandoa walioshikana na kushirikiana....

>KUKUBALI MAKOSA....
Wazee walipata kunena kuwa daima mafahari wawili hawakai zizi moja.......
Maana yake ni kwamba kwenye malumbano hakuna mufaka na makubaliano.....hivyo basi kama umekosa na wewe ni mwanadamu....kwanini usikubali kosa na pengine mtasemeheana na maisha yanaendelea.....!!!!
Unapokiri kosa hata mwenzio anajua kuwa kweli ulipitiwa....lakini unapokuwa mbishi hali ya kuwa ni mkosaji....kunazusha maswali mengi sana kuliko majibu....ambayo yataendelea kuitafuna ndoa yenu na hatimaye kuiangusha.....

Nawasilisha......Elimu hii kwa Wanandoa

🌲🌲Kutoka Pastor Richard Group WhatsApp +255759861768🌲🌲

🌹🌹Sambaza kwa Wezako na kwenye Magroup🌹🌹

Pastor Richard
Kutoka MOROGORO VETA DAKAWA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.