Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 14, 2021

SOMO;URAFIKI, UCHUMBA

SOMO: URAFIKI/UCHUMBA URAFIKI/UCHUMBA NA NDOA NJIA KUMI ZA KIBIBLIA ZA KUMPATA MWENZI WA MAISHA. Mpenzi msomaji hizi ni dondoo tu zilizomo ndani ya Somo hili, nimeona ni vema walau kwa sehemu nikueleze yaliyomo ndani. Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa babaye bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana’.Nianze kwa kusema kuoa au kuolewa ni mpango kamili wa Mungu. Zipo sababu nyingi za kwa nini unahitaji mke au mume tuanze na:- 1. Unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana, 2. Kwa sababu zinaa (1 Wakorintho 7:20), 3. Unapopata mke unakuwa umepata msaidizi na mlinzi. Kibiblia mke /mme mwenye busara mtu hupata kutoka kwa Bwana, maana yake Mungu ndiye anayehusika na kumpa mtu mke/mme. Mungu pekee ndiye anayejua nani ana busara ya kukaa na fulani halafu ndiyo anayekupa huyo mtu. Suala la kumpata mwenzi ambaye hakika ni wa mapenzi ya Mungu kwa mtu husika, imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa vijana na pia wale ambao bado hawajaoa au kuolewa. Lengo la kitabu hiki...