SOMO: SEHEMU YA PILI YA KAZI ZA MALAIKA
ISOMO: KAZI ZA MALAIKA ✔️✔️Part 2 Karibuni Sehemu ya pili mwendelezo wa Somo Hili Uzidi Kujifunza Kwa Habari ya MALAIKA Kule mbiguni Tuliishia Kuwaona WAPELELEZI Kazi wanaoifanya Kule mbiguni.Naitwa Bishop Richard Naekuletea Somo Hili Kwa muongozo wa Roho Mtakatifu katika ufunuo wa juu Kaa Katika Uwepo ili unielewe. 1: MALAIKA WA MOTO Hawa Nia malaika wanaohusika TU na Tanuru la Motoni na SAA nyigine huwatokea WANADAMU kwa muonekano wa moto mfano;Kutoka:3:2 Kutoka 3:2 [2]Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Hesabu 16:35-36 [35]Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba. [36]Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Unapoona watu wa agano la kale walikuwa wakiomba Moto unashuka unateketeza Sadaka au mwali wa Moto hao walikuwa Ni Malaika wa Moto waliokuwa wakishuka nakuteketeza ...