SOMO: MAJUKUMU YA WANANDOA
SOMO; MAJUKUMU YA WANANDOA Naitwa Pastor Richard Mwalimu wa Wanandoa Imekuwa kawaida watu kufunga ndoa saa sita mchana kufika saa 12 jioni ndoa imevunjika. Tena jamii yetu ya sasa iliyomomonyoka maadili na kuingiliwa na utamaduni wa kimagharibi ndio kunachangia zaidi migogoro na mivutano katika ndoa. Kumekuwa na mada nyingi humu zinazohusu ndoa, wengine kuumizwa katika ndoa, wengine kusalitiwa, kupigana mpaka kutoana manundu, wengine hata kuana na wengine kuachana kabisa. Ndio maana nimeona nilete mada hii mezani tuijadili kwa mapana pamoja. Kwa kuanza kwangu kuchangia katika mada hii nitajikita kuelezea majukumu ya mke kwa mume wake na majukum ya mume kwa mke wake. Kwa sababu kila mtu anayeingia katika mkataba wa ndoa, anaingia katika mkataba huo akiwa na matatizo yake binafsi na kiasi fulani cha ujinga wake. Ili ndoa iweze kustawi na kudumu lazima kila mwanandoa ajue wajibu na majukum yake. Wahenga wanasema ndoa ni chuo, hivyo wanandoa wanashauriwa kuwa tayari kujifunza, ndoa hai...