Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 5, 2026

SOMO:TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA

SOMO: TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA WENU ​ Mwalimu:  Pastor Richard (Mwalimu wa Wanandoa) Mahali: Morogoro Veta Dakawa Mawasiliano: WhatsApp +255 710889892 ​        UTANGULIZI ​Karibu katika nakala hii inayoenda kukupa mwanga katika kuendesha uchumba, hasa kwa vijana wetu ambao wapo kwenye mahusiano. Mahusiano mengi yanavunjika na kutokufikia malengo kwa sababu ya ukosefu wa elimu. Nakuandalia mwongozo huu ili kukuwezesha kufikia ndoa yenye baraka na heshima. ​ Maana ya Utaratibu:   Ni makusudi au mpangilio mzuri wa kulifanya jambo liwe katika ubora wa kuonekana vyema. ​TARATIBU 10 ZA KIFUATWA KIBIBLIA ​1. Mruhusuni Mungu Ajenge Uchumba Wenu ​Mnapaswa kuendesha uchumba wenu kwa kutumia akili za Kimungu na siyo za kwenu tu. ​ Andiko: Zaburi 127:1 ​ Mfumo: Uchumba wenu uwe kama   Pembe Tatu (Triangle) . Juu muwekeni Mungu, kulia mchumba mmoja, na kushoto mwingine. Msikaribiane sana kimwili kabla ya wakati; mkikaa mbali na dhambi huku m...