Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 30, 2025

SOMO: MEZA YA BWANA

Picha
SOMO;MEZA YA BWANA. Katika biblia kuna vifungu vinne vya maandiko matakatifu vinavyoelezea vyema kuhusu meza ya Bwana. Vifungu hivyo ni; Mathayo 26:26-29 Marko 14:22-25 Luka 22:15-20 1 Wakorintho 11:23-25 Katika mafungu hayo ya maandiko tunaweza kujifunza mambo mengi,ikiwemo maana halisi ya  “meza ya Bwana  ” ,umuhimu wa meza ya Bwana katika maisha yetu ya sasa, lakini pia damu ya Yesu na umuhimu wake.  Nini maana ya meza ya Bwana? Neno“ Meza ya Bwana ” huitwa pia “ chakula cha Bwana,Karamu ya Bwana, sherehe ya Bwana ” ni Ibada maalumu ya kula mwili na damu ya Yesu ya agano. Ukumbuke,ya kwamba kuna maagizo mawili aliyoagiza Yesu yafanyike mara kwa mara ndani ya kanisa ( agizo la kwanza ni ubatizo na pili ni kushiriki meza ya Bwana Kwa ukumbusho wake). Katika meza ya Bwana kuna vitu viwili; Mkate – kumwakilisha mwili wa Yesu Divai/kikombe cha baraka au kikombe cha zao la mzabibu – huwakilisha damu ya Yesu ya agano jipya Hivyo,meza ya Bwana inaandaliwa na kuhani wa Mungu Al...