SOMO: ISHARA ZA MIGUU KUWASHA
SOMO: ISHARA ZA MIGUU KUWASHA NA MIKONO KIROHO INAASHIRIA NINI. Mungu husema nasi pia kupitia Viungo vyetu Vya Mwili Shida ni kumuelewa. Soma hizi ishara 1. Macho Kucheza Katika ulimwengu wa roho, macho yanawakilisha maono na utambuzi . ➖ Jicho la kulia kucheza:✍🏾 Mara nyingi huashiria habari njema inayokuja, kuona jambo la heri, au kukutana na mtu uliyemtamani kumuona. Inaashiria "maono ya baraka." ➖ Jicho la kushoto kucheza: ✍🏾Huashiria tahadhari dhidi ya habari mbaya, huzuni, au njama zinazopangwa dhidi yako. Ni ishara ya kiroho kukuambia uwe macho na mazingira yako. Mstari wa Biblia:✍🏾 "Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru." ( Mathayo 6:22 ) 2. Mikono Kuwashwa Mikono inawakilisha kazi , mamlaka , na mapokezi . ➖ Kiganja cha kulia kuwashwa:✍🏾 Hii ni ishara ya kupokea . Inaweza kuwa fedha, zawadi, au fursa mpya ya kazi. Ni ishara kwamba mbegu uliyopanda inakaribia kuto...