Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 26, 2023

SOMO:LENGO KUU LA MUNGU KUTUPITISHA KWENYE MAPITO

SOMO; LENGO KUU LA MUNGU KUTUPITISHA KWENYE MAPITO MAZITO. UTANGULIZI.  Inawezekana Kabisa hata wewe saivi upo unapitia kipindi kigumu mapito mazito mpaka umewaza moyoni Umuache Mungu  au Kuona Mungu Amekuacha Nataka nikuambie unayoyapitia Mungu alijua utayapitia kwanini basi ameruhusu iwe pito kwako  kwa sababu kwanza anakupenda na Anaimani kubwa na wewe na anajua hutamsaliti  ni vyema kuendelea kutunza uaminifu wako na Mungu. Karibu ujifunze kupitia Somo hili. Naitwa Bishop Richard nipo Tanzania Morogoro Veta Dakawa  WhatsApp +255759861768 KUNA MAMBO MANNE MUNGU HULENGA KUJIPATIA KUPITIA TUNAPOPITIA VIPINDI VIZITO. 1:KUTUSAFISHA NA KUJIHAKIKISHIA KAMA TUNA IMANI NEYE KATIKA MAJIRA YOTE. Soma: Yakobo:1:2-4 Mungu hutumia majaribu kuchunja watu walio wake na wasiokuwa wake kujua watu wenye imani nayeye kujua watu wake walio wavumilivu ambao wataendelea kumwamini na kumtengemea. Ndugu yangu majaribu hutusafisha na kujua tunapokosea nakutengeneza upya na Mungu tena...