MME/MKE WA SHEETANI ANAVYOKUWA SIFA ZAKE

✍🏾🌳🌳Yajue ndoa/Mahusiano ya shetani Au MTU aliyepewa mke/Mme na shetani Huwa ndoa mahusiano yanakuwa Hivi Soma ujue✍🏾🌳🌳

Muongozo WA Biblia Tunasoma⛪⛪Mwanzo:3;1-9

Katika watoto wengi WA MUNGU wamepokea wachumba  ndoa zilizopangwa na shetani pasipo kuelewa nao wamenaswa katika mitengo hiyo Na shetani saivi Amejinafasi katika maisha yao Baadala Ya MUNGU wetu kushika ndoa zao zimeingiliwa na shetani kwakuwa tu walichangua imladi tu waoane

Haya ndio yanakujulisha ndoa uliyonayo si MUNGU

Mwanzo;2!24

1⃣-Huwa ni watu wasiovumiliana madhaifu yao hawa watu.

2⃣-Huwa ni watu wasioshirikishana  kila mmoja anafanya Yake na mipango Yake. Hawa watu huwa wanasifa hii.

3⃣-Ndani hutawala chuki ugomvi mabishano ndoa hii Haina Amani.

4⃣-Wakipishana kauli tu huwa ni ugomvi hawajui kusameheana au kuombana msamaha

5⃣-Huwa ni watu wanaopishana Imani wanaopishana MUNGU wanaemwabudu mwingine Anaamini hivi mwingine vile hawana imani moja.

6⃣-Huwa ndani kila mmoja Anamaamuzi Yake atakavyo yeye hawana formula ya mke na Mme au sifa ya wanandoa wanasifa ya uzinifu tu.

7⃣-Ndoa yao Inamke Au Mme zaidi ya mmoja inaMungu zaidi Ya mmoja Inamoyo wakupenda zaidi ya mmoja Ndoa huwa inatawaliwa na usaliti haina upendo kabisa.

8⃣-Hawasali pamoja hawaendi kanisani pamoja kila mmoja huyu kilabuni huyu kanisani.

9⃣-Hutawaliwa na ubinafisi sana

🔟-Kila mmoja huwa si mwaminifu kwa mwenzie  na wengine huzivua Pete zao za Agano ili kumweleza MUNGU Mimi huyu nilikosea kwangu si Mme wangu si mke wangu. Wanakaribisha uzinzi.

Neno linasema ;nitakupa WA kufanana nawe nini maana Yake

-Utaendana naye nakupenda na

-Mtasimama katika mwili mmoja uungu mmoja

-Utafurahia na Mtasikilizana ndani

-Mtashauriana na kupeana ushirikiano

Kwanini kwako iwe tofauti ulimpenda kwa ajili ya kitu ndoa si lele mama lazima uyajue haya

Mabint wengine wameokoka wanaolewa na waganga wapinga ramli WA mataifa eti mpaka bint naye Anajiita nimepata Mme mwema wakati Amepewa na shetani.

☝🏽☝🏽Hayo juu niliyoyataja yanaeleza ndoa iliyo ya shetani ndani huwa inasifa hizo

Kama unazosifa hizo Ndoa Yenu Haikupangwa Na MUNGU ulipewa na shetani

☝🏽☝🏽Ndio maana inapingana na neno LA MUNGU lilosema nitakupa wakufanana nawe. Mwanzo.2;18-24 soma mistari hiyo

ADAMU katika orodha ya wanawake wengi alipokutana nao hakuona aliyefanana naye mpaka MUNGU alipoamua kusema naye katika Usingizi mzito akamletea Eva nakumwambia Eva atakufaa hapo ndio alisema huyu ataitwa mke wangu ataitwa mke wangu aliyeumbwa kwa ajili yangu ni mwili mmoja imani moja na Mungu mmoja na Mimi nitajitenga na marafiki makundi wasiooa hiyo ndio itanitofautisha

ADAMU akamjua mkewe akabarikiwa watoto hii ndio Agano LA ndoa

🌳🌳🌳By Pastor Richard

☝🏽☝🏽Mafundisho ya kuepuka ndoa za kishetani au za shetani☝🏽☝🏽

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.