ISHARA NA VIASHIRIA VYA KUJUA MWANAUME ANAKUPENDA HAKUDAGANYI
VIASHIRIA NA DALILI ZINAZOKUJULISHA MWANAUME ANAKUPENDA KUTOKA MOYONI
Naitwa Mwalimu wa Wanandoa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
WhatsApp number Pastor Richard+255759861768
Waefeso;5;23,33
HII MAALUMU KWA WANAWAKE TU
1:ATAKUPA NAFASI KWENYE MOYO WAKE ATAKUPENDA.
Utaona TU hata bila kutengemea amekupigia Simu Amekutumia Sms Amekuja nyumbani Kwenu Amekuletea Zawadi Utaona hata Mienendo Yake atabadilika Mazungumzo Yake utayafurahia ukiongea nae kwenye Simu utatamani Asizime.
2:ANAKUPA MANENO YA KUKUTIA HATAPENDA UPOTEZE FURAHA.
Kwakuwa anakupenda atafanya njia zote ili ahakikishe unacheka au unatabasamu Furaha Yake atahakikisha wewe unafuraha na sio huzuni atakapokuona upo katika Kipindi kigumu atakutia moyo nakukupa nguvu ya Kusimama Tena
Ujue Huyu Ni mwanaume Sahihi
3:ATAWAPENDA NDUGU ZAKO KAMA NDUGU ZAKE.
Kwa Kuwa Amekupenda Wewe ATAWAPENDA na Ndugu Zako na watoto wako atawapenda
Ukiona hii ujue Anakupenda
4:ATAKUFUNDISHA NA KUKUONYA VITU AMBAVYO NI HATARI
Atahakikisha Anakuwa Mwalimu Kwako kukufundisha na Kukuonyesha njia na muelekeo mzuri wa Maisha hatakuacha upotee atakuwa Kichwa kinavyoongoza viungo vingine Atakufundisha Mambo mengi kwenye uchumba TU Utajua kuomba Kwenda katika Imani.
5:ATAKUSAMEHE UKIKOSEA.
Kwakuwa Amekupenda ukimkosea ATAKUSAMEHE.
6:ATAKUWEKA WAZI HISTORIA YAKE YA MAHUSIANO NA KIPI AMEKUPENDEA
Atakueleza kile ulichomfanya mpaka akupende atakupa historia ya Maisha Yake Hatakuficha kitu.
Ujue Huyu mwanaume Anakupenda
7: MWAMINIFU NA ATAKUAMINI.
Atakayekuamini na hatakuchunga au Kukufatilia Mara huku Yupo Kukulinda hapana Usipojielewa Ukavunja uaminifu Ni wewe Yeye atajiaminisha nawewe unampenda
8:ATATUA CHANGAMOTO ILIYO NDANI YA UWEZO WAKE.
Kama utapitia matatizo ujue atakuwa wa kwanza kuyatatua na hata kukopa kwa Ajili yako akusaidie
9:ATAKUWA BABA NA RAFIKI KWAKO
Atakufanya Uwe huru kwake Sio umuongope au mkali mkali TU kila SAA ujue huyo sio mme anayekupenda
10:HATATOA SIRI ZAKO AU MADHAIFU YAKO.
Mwanaume anayekupenda hatawaeleza hata Ndugu udhaifu wako hata Rafiki hawatajua atakutunzia Siri zako
UKIONA MWANAUME ANASIFA HIZI UJUE ANAKUPENDA
Maoni
Chapisha Maoni