SOMO:UASI WA WAUMINI
SOMO: UASI WA WAUMINI NDANI YA KANISA LA LEO.
Hesabu;16 yote soma
Naitwa PASTOR RICHARD NINAKUKARIBISHA KATIKA SOMO HILI NIFATILIE KWA UMAKINI SOMO HILI UKATUBU ULIPOASI NA KWENDA KINYUME NA MAMLAKA ALIYOIWEKA KWAKO MUNGU KAPOKEE.
MAANA YA UASI ?
Ni kwenda Kinyume na Mtumishi aliyekupa Mungu Akuongoze au Akulee Kiroho.
KUASI ni Kitendo cha Tofauti na mtu unapotenda dhambi au uovu Yenyewe Kuasi hulenga Kwenda Kinyume na Angizo lilotolewa na MAMLAKA au Mamlaka husika
Mfano; Ccm na chandema mbuge wa chandema alihamia Ccm akaanza Kumkashifu kiongozi wake. Huo ndio UASI.
Muumini aliambiwa Na Baba Yake wa Kiroho awe anafanya usafi na Kupamba Kanisa Yeye akaenda Kuwaambia WAUMINI wezake mchungaji Amemtongoza Amemwambia anakuja kufua nguo na Yeye ndiye mke mtarajiwa Tayari unakuwa umeasi.
Mchungaji alitangazia watu wote wafunge nakuomba lakini mimi sikufunga tayari umeasi.
Kuasi nikitendo cha Kupigana na Mtumishi wa Mungu aliyebeba maono yako akufikishe kanani Hebu soma hesabu;16 Uone Kora alivyoanza kuasi.
MADHARA YA KUASI
●Utaangamizwa na Mungu wewe na UZAO wako.
●Utatengwa na MAMLAKA iliyobeba maono yako kwa hiyo hayatafika mbali.
Mfano ukianza kumpinga mchungaji ujue wewe hautafika mbali lazima uanze kupingwa umedharau na kuasi MAMLAKA aliyokupa Mungu.
●Utakuwa Mtu utakayejiona Upo sahihi Katika Uasi wako kumbe umekosana na Mungu
●Mungu atakuacha na Mkono wake utandoka kwako.
●Mungu atamruhusu Adui aanze Kukushambulia.
NINI Tufanye Sasa Tulioasi.
●Tumrudie Mungu kwa Toba ya Kweli.
●Tuwatii Watumishi waliowekwa mbele Yetu Tusianze Kuasi.
●Tusianze Kuwashambulia Kwa Kuunda vikundi vikundi ndani ya Kanisani Vyenye Anjeda Ya Kupingana nae.
●Tuikemee dhambi ya UASI iachie kanisa.
NITATOKAJE SASA KAMA NIPO KWENYE UASI
●Utaingia maombi Yatoba yenye Kumanisha Siku Tatu Kwa Kutokufunga Uwe na Sadaka Yako ya siku ya kwanza siku ya pili na Tatu Utaomba Kadiri roho anavyokuongoza uutubie uasi wako uliofanya Sadaka hiyo Toa Katika hiyo madhabahu uliyoiasi
HITIMISHO
OMBA HIVI.
Baba nakuja mwanao Richard nimekutenda dhambi baba yangu wa kiroho niliasi aliponiambia Tufunge mimi sikufunga aliponionya mimi nilimchukia nisamehe nisamehe Nisamehe Baba Mimi mwanao Nimekosa nimekosa mimi Na nafsi yangu kuanzia Leo sitaitwa muasi Katika jina la Yesu. AMEN
RUDIA MARA 3
WITO
KWA MASWALI ULIZA KWA KUANDIKA CHINI YA POST HII.
WHATSAPP PASTOR RICHARD +255759861768
Maoni
Chapisha Maoni