SOMO;JITUNZE na Jisimamie
✍️SOMO:✍️MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOJITUNZA NA KUJISIMAMIA KIROHO FATA HAYA
Karibuni Leo Nataka Tufundishane Nguvu ya Kujisimamia wenyewe nakutunza maisha yetu kiroho
Kunawatu Wapo wanatamani wasimame watembee wao Kama wait lakini hawawezi kila wakijaribu Kujitunza kiroho wanajichafua Tena kila wanapojichafua Shetani na mapepo yanapata kuwatesa wachawi wanawatesa Kumbe Ni Mtu kuuchafua maisha yake ya kiroho .
Sasa Leo Nataka Ujifunze na Ujue Ufanyeje ili usimsme usiyumbeyumbe na Tatizo lako lisikurudie Tena fata haya Kwa Majina Naitwa PASTOR RICHARD Nipo Morogoro Veta Dakawa nchini Tanzania
Vitabu rejea;1 Timotheo;4:16 Kutoka;23;21 Ayubu;32:13 Torati;11;16 Soma Vitabu TAFAKARI Kisha endelea kusoma
KUJITUNZA Ni Nini Kiroho; Ni Hali yakuishi maisha yasiyo na Mawazo machafu au Kusema Mungu Hawezi. Macho yako yaone ukuu wa Bwana.
KUJISIMAMIA NI KITENDO NGANI: Ni Hali ya kuhakikisha maisha yako Mawazo yako na Moyo wako vinamwabudu Mungu nakuchukia Mambo yanakufanya ujichafue Sifa ZaKo njema za mtoto wa Mungu kuhakikisha Unapenda Ibada kuomba Kujifunza Neno.
✍️✍️SASA NAFANYAJE ILI NIJITUNZE KIROHO ??
Swali nzuri Sana Unachotakiwa Cha Kwanza Ni wewe mwenyewe Kujitambua nakuelewa uhusiano wako na Mungu wako ukoje.
1;Ukijua uhusiano wenu hutamsaliti Wala kumhudhunisha sababu wajua Mlivyoanza mahusiano mpaka Kufikia kuokoka au kuwa hapo ulipo Leo.
2;UKijua Lazima Ujue Kwanini Uichukie Dhambi na Kwasababu ngani umeokoka majibu na maswali haya ujihoji na Ujue Ukipata jibu utakuwa umesongea hatua Kubwa Ya Kwenda kusimama mwenyewe
3:Tafuta Baba wa Kiroho na Hakikisha unatoa Fungu la kumi maana linawajengea uhusiano wenu na Mungu uzidi kukua nakupendwa Kupitia Zaka hakikisha unakula chakula Cha kiroho na kujifunza mengi chini ya Baba yako wa Kiroho.
Utakuwa umejitunza Sasa mpaka hapo hatua inayofata kusimamia Mafundisho ya Baba Yako wa Kiroho ili uzidi Kushinda na Kug,ara Kama Nyota ya Alfajiri.
✍️✍️SASA FANYA HAYA ILI KUJISIMAMIA MWENYEWE.
1:Tayari hakikisha unaebaba wa Kiroho kabla yakutaka Kwenda TU peke yako hutaweza Kujisimamia Pasipo Mlezi wa kiroho Tena awe na ujazo wa Kiroho ule na Kufundishwa Neno la Mungu uridhike ushibe kiroho.
2;Penda Mafundisho nakujifunza Kutoka Kwake Kwa Kutumia muda wako Kwenda kanisani na Kumweleza unapokwama kiroho.
3:Amini moyoni mwako unaweza Kujisimamia na Kuendelea
4;Mfanye Baba Yako wa Kiroho Kama mshauri TU usimsujudie nakufikia hatua Kama Yeye hayupo kanisani huedi au Kuona Yeye TU kila kitu unakimbilia Kumweleza hapana tabua yule Yupo kwa Ajiri akuongoze kiroho nakukumwangilia ukue kiroho. Usimuache Mungu ukaanza kumuona Yeye ndio Mungu wako.
5;Tulia MADHABAHU moja TU na Usiwe na Wababa wa Kiroho wengi au MADHABAHU Nyigi unazozitolea Fungu la kumi Hali hii Ni hatari kiroho hata katika Kupoteza Ulicho nacho ndani yako au kupigwa na adui.
Tulia Sehemu moja na hudumiwa Sehemu moja kula chakula Sehemu moja ukiwa unamadhabahu Nyigi utanaswa na MADHABAHU za Shetani.
MAMBO MHIMU YANAYOKUKUZA KIROHO
1; Shuhuda mbalimbali
2; Masomo mbalimbali ya Neno la Mungu na maisha ya Duniani
3;Maombi Kujifunza Kuomba mwenyewe
4;Ibada na Sifa Mbalimbali kusifu.
5:Majaribu na Mapito
6;Kukumbuka historia yako.
Haya yanakukunza haraka kiroho unajua kusimama mwenyewe
Hitimisho ✍️✍️
Tunapaswa Tujitunze na kusimamia utakatifu na maisha yetu yasiteseke au kumpa nafasi Shetani katika Mawazo yetu na akili zetu
Nawatakia ushujaa mwema was Imani
Ni Mimi Mjumbe Mwaminifu wa Kristo Pastor Richard
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na Ushirika wa ROHO MTAKATIFU uwe nanyi Leo hata milele.
Watumie Wegine
@2020 Pastor Richard
Maoni
Chapisha Maoni