SOMO: WAJIBU WA MTUMISHI WA MUNGU NI KUWAFUNDISHA WATU
✍️SOMO: ✍️WAJIBU NA JUKUMU KUU LA MTUMISHI WA MUNGU.✍️
Tufunue. Biblia 1Timotheo sura ya:4'na 5 Soma Yote
Kisha TAFAKARI Neno Ukishasoma Mistari hiyo.
Kuna Wakati Watumishi wanapaswa wakumbushwe Kazi Kuu waliyoitiwa ndani Yao na wajue wajibu wao kwa washirika wao Hata Kondoo wao
Pia Na Watoto (waumini )wanapaswa wajue wajibu wao Wanapaswa wafundishwe nakuelekezwa wapaswayo Kufanya na Jinsi yakusimama wao wenyewe Kutatua Matatizo na Kukua kiroho"Ni wajibu wako mshirika kupenda Mafundisho na Kufanyia kazi.
Lengo La SoMo; Kuwakumbusha Watumishi wajibu wao na wanafunzi wajibu wao
Dhima Yetu MOTO WA YESU; Kuadaa Watumishi wenye nguvu ya kiroho
Na Hofu ya Mungu.
WAJIBU WA MTUMISHI NDIO NINI,,? Ni Hali inayomfanya Mtumishi ajue kusundi la Mungu ndani yake Nini Ili Kumsaidia Asikengeuke au Kupotosha Kundi au Kondoo Kuwatawanyisha.
KUNA WAJIBU AU KAZI MBILI TU ALIOPEWA MTUMISHI WA MUNGU
1;WAJIBU WAKE WA KWANZA; KUFUNDISHA KUNDI.
Mtumishi anawajibu na Kazi kumbwa Kulifundisha Kanisa au Washirika wake Katika Mambo ya Kiroho na Mwilini.
Mambo MHIMU Mtumishi afundishe
1;Nguvu ya Kumtengemea Mungu na Jinsi Anavyotenda kazi
2;Awafundishe watu wakiri Mungu Anaweza Hashindwi
3;Sauti ya Mungu na Jinsi yakuielewa
4;Kufanya kazi zao kwa Kumtengemea Mungu
5;Roho Mtakatifu na Anavyotenda kazi ndani Yao
6:Maadili Na Utoto mwema Wa Mungu
7;Kusundi la Mungu ndani Yao na Jinsi ya kuwasaidia Kufikia kusundi
8:Maisha ndani ya Wokovu na Maisha ndani ya Dhambi
9;Kutatua Na Kuomba wao wenyewe kujisimamia Vizuri.
10;Fundisha Mambo kwa Kufata majira na wakati uliopo
2;WAJIBU WA PILI;- KUELEKEZA KUNDI NA KUONYA KUNDI.
Mtumishi unatakiwa uwaelekeze watu na kuwaongoza katika njia zuri ya Ufalme wa Mungu nakuwatia nguvu nakuwaonya wanaoenda nje ya mstari wa Mungu watengezenee moyo uliojitoa kwa Mungu.
Mambo unayopaswa uelekeze Mtumishi
1;Kazi Za Kufanya Zenye utukufu wa Mungu.
2;Mienendo na utulivu ndani ya Yesu Faida Yake hasa Vijana Kaa nao.
3;Imani na Nguvu zake ndani ya Mtu.
4;Utume na uijilist mitaani na maeneo Yote
5;Injili na Ushuhuda,Miujiza ya Yesu, ili wasipotee
6;Maombi ya Vita na Jinsi ya Kumuomba Mungu Anajibu
7;Maisha ya ndoa na Uchumba kwa kijana sayuni
8;Maisha Bila Elimu na Kazi yanavyokuwa shida
9;Malezi ya watoto na njisi Kutunza mazingira Yao
10;Elekeza na mengine Yote ili kumfanya mtu ajue nakutambua madhara Yake.
WAJIBU WA MUUMINI
1:Kupenda Mafundisho ya Neno la Mungu
2;Kufata na Kutii Anachofundishwa na Kuelekezwa
3;Amtii na Kumheshimu yule anayemuongoza kiroho
4:Ajue mchungaji Yupo kwa Ajili ya kumfikisha Mungu anapotakiwa afike
5;Awe tayari na kujitoa Kwa Mungu
6;Atumike Sawasawa na Karama Yake
7;Awe Mwaminifu wa Zaka
8;Aombe ushauri nakumweleza Baba Yake wakiroho
9;Atafute Nakala Na Masomo mahubiri mbalimbali Soma Vitabu ujifunze zaidi
10;Tulia na Ujitunze ndani ya Yesu.
Na Hitimisha Kwa
Kumshukuru Baba Mwana na ROHO MTAKATIFU kwa Kunipa Kuliandaa SoMo na Kuliwasilisha kwa wahusika Ili Kufikisha Kanisa linapotakiwa.
Ansateni wote mnaoendelea Kujitoa kwa Mali zenu na Ushauri wenu ulionifikisha Leo hapa Mungu Azidi kuwaangazia Nuru mbele Yenu.
WITO
Maisha Bora Ni kuwa na Yesu Uokoke na uwe na Baba wa Kiroho anayefanyika kuwa Baraka Heshimu Sana yule anayekuongoza kiroho maana huwezi fanikiwa endapo kiroho hujafanikiwa
SIMU ZA MAOMBEZI
Kuongea na Bishop Richard nikuanzia Saa:12;00jioni mpaka 8;00usiku
Piga namba+255759861768
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni