✍🏾🌳SOMO; NGUVU YA MSAMAHA 🌳🌳✍🏾

✍🏾🌳SOMO; NGUVU YA MSAMAHA 🌳🌳✍🏾

Vitabu Tufunue Tusome Marko:3;29 Matendo;5;31 Daniel;9;5_10 Zaburi;130:1_6

UTANGULIZI;
Kuna Mtu Ambaye Anaweza akawa Anateseka Kisa moyo wake hajui kusamehe na hajui madhara ngani Ambayo Anayapata asippsamehe mpaka mwingine SoMo Hili Limemwinjia majibu Yake kayazuia Mungu asimjibu kisa Msamaha Leo Nataka Kumponya Mtu wa hivi ili Akashuhudie Hakuna Kukaa Unasoma Shuhuda za wengine Lazima hiyo kamba iliyokufunga inayozuia muujiza wako INAYOKUFAnya ukosane Na Mungu Kila siku umebebelea mafurushi ya mizingo ambayo uwezo wako huwezi lakini ndio umekuwa mtaa mzima wanakujua husamehi wengine Kila ukikosana mchumba wako mmeo mkeo bos wako hujawasamehe Ndio chazo hupati Tena kazi kwingine Mungu unamuomna kanyamaza ,,,,,,,,
Endeleaa Upone Ufunguliwe usijifunge Tena

Naitwa Pastor Richard Naishi Morogoro Tanzania
Ni Askofu na mwanzilishi wa ya Huduma ya Roho Mtakatifu yaani Holy Spirit Ministry
Yenye Office zake Kuu
Zipo Nchi ya Tanzania Mkoa wa Morogoro Wilaya ya Kilosa Kata Ya Mbingiri Kijiji Cha Mateteni Office na Kanisa Hili Lipo nyuma Ya High school

KWA Wageni Mnaofika Fata Maelekezo Haya
Panda Magari ya kuja Morogoro Shukia Msamvu sted hii sted ya Mkoa
Ukishuka hapo chukua gari za kuja dumila waambie nishushe veta Dakawa ukishuka chukua pikipiki waambie nipelekeni kwa Pastor Richard au Kanisa la Moto wa Yesu au Moto wa Yesu Utaletwa

Beba notbook peni Biblia Yako Utakaa siku 3 pakulala papo kula utajigharamia Mungu atakuhudumia ukikanyaga MADHABAHU ya Moto wa Yesu Kupitia Neno la Mungu Tu.

Karibuni Wote MADHABAHU ya Moto wa Yesu
Simu za kuongea na Pastor Richard+255759861768

Somo Letu Tunaendelea Linaitwa NGUVU YA MSAMAHA;

Msamaha Nini Kwanza;
Msamaha nikufutiwa makosa yako maana Yake msamaha inatolewa kwa mkosaji TU
Nisamehe Maana Yake Kutambua Kosa Wewe mkosaji hutarudia Tena Kosa ndio maana ya Kusema Nisamehe

Maneno haya hutumika kwa mkosaji na Aliyekosewa Pia huwa uponyaji kwao Pande mbili Zote na huwa mlango wakufungulia majibu Kwao.

Lakini Kwa MTU ASIYESAMEHE AU ANAESEMA NIMESAMEHE HALAFU BADO ANAKISASI HUWA MLANGO WA YEYE KUINGIZA MATATIZO NA MAGONJWA MINYORORO NA KUMFANYA MUNGU ANYAMAZE KABISA

Nikuulize Mwanangu KWANI WEWE UMESAMEHE CHUNGUZA MOYO WAKO NATAKA UFUGULIWE LEO HII SITAKI UTESEKE INATOSHA.

Kuna Makundi Mawili TU YA MSAMAHA
1;Msamaha Wa Mungu
Huu msamaha hulenga wewe mwanadamu umemuacha Mungu umekuwa ukiabudu miungu kusononeka kunug.unika na Kumkufuru Mungu kwanini Alikuumba Kitu Ambacho huwa dhambi kumbwa
Umetoa mimba umeua watu kwa Maneno ya uchonganishi Umekuwa mchawi hutaki kuacha Utubu uache Uzinifu uache ulevi uache Bangi

Ujue Upo Katika Kosa La Kuvunja Amri kumi na sheria za Mungu pia Kuharibu kabisa Uhusiano wako Na Mungu

Ufanyapo haya Ujue wa mkosea Mungu Sana
1;Kusononeka
2;Kunug.unika
3;Kumkufuru
4:Husamehi
5;Kuabudu miungu
Yaani saa nyingine unawaza kwanini Mungu Alikuumba kwanini Upo hai kwanini Upo na umbo la hivyo au sura unajiona Mungu alikukosea

Wamuuzi Mungu na kumfanya ANYAMAZE  Asijibu

Faida Hizi Unazipata Leo Utakapopatana na Mungu

1;Kufanywa kuwa mmoja ya wanafamilia Mbinguni
2;KUJIBIWA Maombi Yako
3;Kupewa Moyo wa Kuwapenda wengine na Kuwathamini
4;Kumshawishi Mungu Anasikiliza Maombi yako.
5;Unaponywa magonjwa Yako Na Matatizo Yako
Soma Zaburi;103;1-6
6;Baraka Milango ya Baraka itafunguliwa
Uchumi wako wateja Pesa miladi nk Soma Zaburi;103;5

HASARA zake Utakazopata Ukiwa Hujapatana Na Mungu hajakusamehe

Utajiona Unadalili Hizi
1:Kukosa Amani na Furaha Utakuwa mtu wa Mawazo na huzuni yaliyoabatana nakukata Tamaa

2;Magonjwa Na Kudhulumiwa Kutapeliwa Kufukuzwa kazi kupoteza vitu
Utajiona Hizi dalili Unazo ujue Hujapatana na Mungu.

3;Utakuwa na Moyo Mgumu kusamehe wazako Utakuwa kila ukifikiria unayaona mabaya ya wezako TU madhaifu Yao na Hutasamehe kabisa
Ujue wewe umekosana na Mungu msaha TU

4:Utafanya Mungu ANYAMAZE mpaka utajiuliza hivi kwanini Mimi Mungu hajibu kumbe Husamehi wengine Hujapatana nae

5;Majanga ya Vifo na Magonjwa yataandama familia yako mkeo mmeo watoto
Rudi magotini Anasikia Atakusamehe

2;Kundi la Pili Ni Msamaha Unaolenga Mwadamu anaomba Msamaha kwa Mwadamu mwezake
Yaani namanisha Mimi Pastor Richard nimekukosea Wewe Mwanangu nakuja kukuomba Msamaha.
Mathayo;6;14-15 Usome Sio Mistari ya Biblia Unakuwà hufunui namaana kukuwekea Mistari Usome

Huu Msamaha huwalenga watu wawili Lazima mmoja Wapo awe Mkosaji Mwingine aombe msamaha

Faida Hizi Au Dalili Hizi utaziona endapo unafuta makosa nakumuachia Mungu Tu sio kumfikiria mtu unajipa stress za Bure
1;Utasemehewa makosa yako Utapatana na Mungu
Ukijua kumsamehe TU unayemuona kwa macho ujue wewe Mungu umepatana nae

2;Utapata Amani moyoni hata ukikutana nae Hutakuwa na chuki
Ujue Wewe Unajuakusamehe hii inamfanya Mungu akupende

3;Utajenga pakubwa Sana Upendo utauweka uwe ndani Yenu na hii huwa ndio Sifa kuu ya Mungu Upendo yaani utamuaibisha Shetani na mapepo Yake hamtakosana Tena maana Utakuwa umejenga upendo.

4:Utajibiwa Maombi yako Utamfanya nakumshawishi Mungu akujibu
Ndio maana Utaona watu ambao hawajaokoka wanajibiwa sababu wanajua kusamehe watoaji na wanaupendo Mtu yeyote mwenye upendo na mwezake atamshawishi Mungu amjibu ombi lake.

5;Utaponywa magonjwa yako mizingo utatuliwa😍🙂🙂

HASARA UNAZOZIPATA USIPOSAMEHE WENGINE.

1;Mungu Atanyamaza Kabisa Utaombewa na utafunga Mungu atajibu mengine TU sio ombi lako la mhimu hutaaona anajishughulisha
Kumbe Hiyo inakuwa inakufundisha Samehe pia ondoa kunug.unika kuabudu miungu yaani kwenda kwa WAGANGA  Kumkufuru Mungu yaani unajikosoa ulivyoumbwa acha___Acha.

2;Utakuwa na Moyo wa Kumchukia uliyekosana nae unajua Kuna watu wanaumwa presha humu Dawa Yao hawasamehi wengine wanateseka humu Hawajibiwi Tatizo lao kubwa Ni Msamaha TU
Ukitembea moyo unachukia wezako unajenga kisasi na mauaji ya nafsi ndani yako nakuwaza Mambo mabaya juu ya adui zako.

3:Hutafunguliwa katika magonjwa Uchumi Nk Utaombewa matatizo unayarudisha kwa moyo wa kutokusamehe wengine watakuwa wanashuhudia wewe bado

4:Utajenga Uadui na kisasi juu ya mkosaji wako
Kwanini uteseke Kwanini Leo hii usitue mzingo huu

Nataka uponywe Nataka nikuone ukiniletea Ushuhuda
Nasema nawe usiyesamehe wengine

Na Usipo ponywa na ukabadilika na SoMo Hili
Basi Utakuwa unamatatizo ya ufahamu sababu Neno huponya
Neno Hufanya magumu Yawezekane

Njisi Ya Kupatana na Mungu Fata hatua Hizi;

1;Samehe na kufuta makosa ya wengine usiwaze ndani yako.
2;Ingia chumbani kwako au Sehemu palipo na ukimya
3;Pinga magoti Kisha ikusanye mikono yako shika kitovuni au kifuani.
4;Anza Kuomba Ukinyenyekea shuka chini ujione wewe mkosaji mbele za Mungu mweleze ulipomkosea
5;Tulia Dakika Tano Kumi Ukiwa kimya katika utulivu Atazungumza nawe nakukupa Maelekezo sikiliza Kwa Umakini utakapokuwa unaswali uliza kwa kutamka utaisikia Sauti ndani ikiongea Tena vizuri

Nawatakia Wote Mfunguliwe Wanangu wote ndani na nje
Endeleaa kuwahubiria wengine wanaoteseka waliongiza waje kwenye nuru wafurahie

Ni Mimi Mtumwa wa Kristo kwa watu wote Pastor Richard Kutoka Morogoro veta Dakawa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.