NGUVU YA MWANAMKE MWENYE HEKIMA

⌚✍🏾✍🏾SOMO; NGUVU YA MWANAMKE MWENYE HEKIMA HUJENGA NDOA YAKE LAKINI MWANAMKE MPUMBAVU HUKIMBILIA KUIVUNJA NDOA YAKE HALI KADHALIKA MWANAUME MPUMBAVU HUTOA TARAKA ASITAFUTE SURUHU NA MKEWE KWA KUKOSA HEKIMA HUONA SAWA TU.✍🏾✍🏾✍🏾

MITHALI;14;1_13 1wakoritho;11:1_15 Waefeso;4;4

Karibu Mwanangu ujifunze Somo Hili litakalo kufanya uvue upumbavu ukavae vazi la hekima nakutulia na ndoa yako uchumba wako na msimamo wako.

Naitwa Pastor Richard Ni Bishop Richard Muasisi wa makanisa ya Holy Spirit Ministry Tanzania Moto wa Yesu yaliyopo nchini Tanzania na makao makuu Yake ofsi zipo Morogoro wilaya ya kilosa kata ya mbingiri Kijiji Cha Mateteni

Lengo Kuu LA SOMO LETU; Tufikiri Kila maamuzi Tunayoyafanya yanaleta Faida Baadae au Yatatupelekea Kuteseka Tusiamue Vitu Kwa Hasira au Kukomoa mtu.

HEKIMA Ni Nini Ni kufanya Mambo kwa utaratibu au usawa bila kupendelea
Upambavu Ni Nini Ni kufanya Mambo ovyo ovyo bila usawa Wala mpangilio wowote
Mwanamke Ni kiungo Cha mwili katika mwili wa mwanaume
Mwanaume nae Ni kiungo Cha mwili katika mwili wa mwanamke

Kiungo kimoja chatengemea kiungo kigine ili kuupamba mwili na kuufanya mwili wako Ufanye kitu chochote kwa maamuzi yoyote lazima viungo vishirikiane ndipo patakuwa na usawa wa kuleta maamuzi.

Ndoa nyigi huwa hazichukui mfano wa viungo katika mwili au mwanamke kutokutambua Mimi Ni Nani au mwanaume kutokutambua ndani ya Nyumba Yeye Ni Nani

Hufanya mmoja aseme Mimi Ni mkono bila Mimi atashika kitu nakufanya kitu

Mwingine aseme Mimi Ni macho ndio mhimu ataonaje nakukifata kitu bila Mimi kuwepo

Mwingine atasema Mimi si mguu niondoke Sasa tuone Kama atasimama peke Yake bila mguu

Mwingine ndani ya Nyumba Anasema Mimi Ni mdomo nikiondoka atakula wapi hata Kama anamajuba Yake atakula magari Yake au Mali zake Kila mtu ndani akianza kujiona Yeye Ni kiungo Bora zaidi yako nakujigamba hilo huwa lango linaenda kubomoa maana ya mwanamke ndani maana ya mwanaume ndani kitu kitachofata Ni mji kujawa Kukosa Amani na ugomvi usioisha.

MATOKEO YA KUJIONA WEWE NI KIUNGO ZAIDI YA MWINGINE KWA WACHUMBA NA WANANDOA.
1;Nyumba hujazwa Ni upumbavu na ujinga wa kila namna
2:Mambo Yenu hamtashirikishana kila mtu atafanya peke Yake
3;Mtakuwa na Ugomvi wa kila siku na matusi ya nguoni yasiyoisha
4:Nyumba itajazwa kashifa mbalimbali na Maneno kila Leo
5;Mmoja atataka aonekane Yupo juu katika Mambo Yake zaidi ya mwingine
6:Hata Neno msamaha halitatamkwa au Kusikika wataishi maisha ovyo ovyo haitaeleweka Nani mwanaume au mwanamke
7;Amani hutoweka ndani ya mahusiano Yenu
8:Uaminifu huwa zwiro Hakuna Uaminifu.
9;Kila mmoja huwa na maamuzi Yake ndani SI anajiona Yeye kiungo Bora zaidi.
10;Ndoa huvunjika tu au mahusiano hayadumu

Dalili Hizi ukiziona Unazo ndani yako ujue umepoteza Kitu kinachoitwa hekima ndani Umekaribisha upumbavu utawale Hali itakayoharibu nyumba yako ndoa yako

Anza Kujenga Sasa

Naitwa Pastor Richard
Morogoro veta Dakawa
Simu+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.