SOMO : MJAMZITO NA TENDO LA NDOA

*SOMO:MJAMZITO NA TENDO LA NDOA*

Pastor Richard

Darasa La Wanandoa

Simu +255759861768

👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽

Wakati wa ujauzito wanawake wengi hukosa hamu ya tendo la ndoa hivyo mwanaume unahitaji kuwa na mawasiliano mazuri ili mambo yaende vizuri.

*Je, Mwanamke mwenye mimba anaweza kuendelea na tendo la ndoa* ?

Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba tendo la ndoa kwa mwanamke mwenye mimba ya hatua yoyote ya ujauzito inaweza kumuathiri mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni ( fetus)
Hata kama kunatokea  miscarriage bado sayansi inathibitisha kwamba chanzo huwa si sababu ya tendo la ndoa wakati mwanamke ana mimba, bali sababu zingine kabisa.
Tafiti nyingi zimefanywa kwa kufuatilia wanawake ambao waliendelea na tendo la ndoa huku wakifika kileleni ( orgasm) na wale ambao hawakuwa wanafika kileleni wakati wa tendo la ndoa, na wale ambao hawakufanya kabisa tendo la ndoa muda wote wa ujauzito.
Matokeo yalionesha kwamba wanawake wote walizaa watoto ambao hawana tofauti yoyote kiafya.
Hivyo tendo la ndoa ni salama kabisa muda wote wa ujauzito.

*Je, ni wakati gani huruhusiwi tendo la ndoa wakati wa ujauzito* ?

Ni pale tu mwanamke anapojisikia kuwa na  bleeding au maumivu yoyote au  leakage ya majimaji yajulikanayo kitaalamu  amniotic fluid.
Mwanamke mwenye mimba haruhusiwi kuingiza upepo ( by forcing) kwenye uke wako kwani husababisha kitu kinaitwa  Air bubble kitendo ambacho kinaweza kusababisha kifo kwa mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni kwani  hu-block mishipa ya damu. Wapo wanaume huwa na mchezo wa kubusu huku wanapuliza huko bondeni ( afrika ya kusini) kabla ya kuanza kuchima dhahabu.
Pia kama mmoja ya wanandoa ana magonjwa ya zinaa (STD) haruhusiwi tendo la ndoa hadi daktari athibitishe kwamba amepona ama sivyo anaweza kusababisha mtoto tumboni aambukizwe.
Pia kama una historia ya tatizo la cervix

*Kumbuka* !

Pia ifahamike kwamba si wanawake wote wakiwa na mimba hupenda tendo la ndoa wengine huwa hawapendi kabisa.
Utafiti unaonesha pia kwamba mwanamke mwenye mimba hukosa hamu ya tendo la ndoa miezi mitatu (3) ya kwanza,  then hupenda sana tendo la ndoa miezi mitatu inayofuata na Pia miezi mitatu ya mwisho hukosa tena hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya saikolojia ya kusubiri mtoto kuzaliwa.
Ingawa uzoefu unaonesha kwamba mwanamke mwenye mimba husisimka haraka na kufika kileleni mapema sana kwa sababu damu huwa nyingi sana kuzunguka uke na hivyo kuwa  sensitive zaidi kuliko akiwa hana mimba, pia ni dhahiri kwamba mwanamke anayefurahia tendo la ndoa wakati ana mimba hupata utamu wa uhakika.Kitu cha msingi pia ni kuzingatia mikao au milalo wakati wa tendo la ndoa kwani mwanamke mwenye mimba anahitaji mikao au milalo ambayo haikandamizi tumbo lake.
Hakikisha mnakuwa na  communication nzuri kuhusiana na suala la tendo la ndoa ili kila mmoja aweze kuwa msaada kwa mwenzake

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.