MAOMBI YA MWANAMKE BORA WA KWENYE NDOA

*MAOMBI YA MWANAMKE BORA MWANAMKE MWEMA KWENYE NDOA AOMBE HIVI.

Pastor Richard

Darasa La Wanandoa

Simu +255759861768

👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Mwenyezi MUNGU, Mfalme wangu uliye juu..binti yako ninashukuru kwa kunipigania mpaka muda huu. Nimepitia mengi na bado ninapitia kila aina ya majaribu lakini unazidi kuniimarisha. Wakati wanawake wengine wakilalamika, wakilia, wakikashifu na kudhihaki mimi nimechagua kukimbilia kwako. Ninapenda kukuabudu na kukutegemea wewe na sio kumtegemea binadamu!
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Wanawake wenzangu wengi wanahangaika na ndoa zao, wamepoteza tumaini la maisha na mahusiano, lakini mimi sitakata tamaa; nitakukimbilia wewe.
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Nashukuru sana kwa namna ulivyoniinua. Je ni nani kama wewe? Kila nikijitazama aina ya mwanamke ambae nimekua, sababu kubwa ni wewe. Umenifanya niwe mzuri, ninayevutia, smart na kila aina ya sifa anayotakiwa kuwa nayo noble woman!
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Nipe busara ya kuishi na mume, wanawake wengi tunashindwa kuangalia udhaifu wetu na kutupia lawama udhaifu wa waume zetu; ila mimi sitafeli katika mtego huo. Nipe ujasiri wa kujishusha na kukubali kurekebishwa na nipe uwezo wa kurekebishika!
👇🏽👇🏽👇🏽
Mtumie mume wangu kunirekebisha pale nitakapokua nakosea. Nijaze roho wako. Maana wewe mwenyewe ulisema utatuletea roho mtakatifu awe msaidizi, basi na aje katika maisha yangu ili na mimi niweze kumsaidia mume wangu katika kazi, na harakati za kimaisha!.
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Nifundishe namna ya utii. Maneno yako yanitengeneze ili nikue kiimani kwa maana kadiri nitakavyokuwa nakua kiimani ndivyo nitakavyozidi kuwa mke na mama bora!
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Tengeneza ulimi wangu, nipe busara ya kuzungumza ili maneno yatokayo kinywani mwangu yasiharibu nyumba yangu. Maneno yangu yasimuudhi mume wangu, watoto na ndugu watakaonizunguka!
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Nitakapokua na hasira, nitulize kama ulivyotuliza dhoruba ya bahari..nisaidie ku-control hisia zangu..nisaidie kuniweka mbali na hisia za usaliti, uongo, na kila aina ya uharibifu. Naamini kwamba Peace is my portion, my home will be a home of joy.
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Bariki watoto watakaotoka tumboni mwangu, watoto wangu wataniita mbarikiwa na mimi nitawaita baraka. Kila asubuhi nitazungumza nao kuhusu maisha na kuwasaidia wakue kwa akili na kimo wakikujua wewe Mungu wangu! Nifundishe busara ya kuwasikiliza wanangu, mimi ni mama, umenipa jukumu la kulea. Zuia kabisa ulimi wangu pale utakapotaka kuzungumza maneno makali yasiyo na staha kwa wanangu maneno ambayo yanaweza kuwavunja moyo. Nipe ushauri bora na mimi nitawashauri vema!
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Nisaidie kutunza nyumba yangu. Nipe uwezo wa ku-control mood ya nyumba ili mume na watoto waone ndio sehemu salama kwao kila wakati. Mfundishe mume wangu namna ya kushirikiana na mimi. Tusaidie uwezo wa kufanya maamuzi sahihi yenye tija kwa familia yetu, ndugu, jamaa na marafiki!
👇🏽👇🏽👇🏽
Tupe mimi na mume wangu nidhamu ya matumizi ya fedha, tujalie ubunifu wa vyanzo vya mapato na bariki kazi za mikono yetu!
👇🏽👇🏽👇🏽
Kuhusu tendo la ndoa, nisaidie na niimarishe nizidi kuwa na mvuto kwa mume wangu ili asinichoke na daima afaidi mke wa ujana wake. Bariki ‘intimacy’ yetu na bariki tendo letu la ndoa ili lisifanyike kwa mazoea bali kama namna ya kuzidi kuimarisha ‘bond’ yetu!
👇🏽👇🏽👇🏽
Lord, cover my life, fight my spiritual and physical battles. My marriage will give You glory because You, my husband and I will make a formidable team.

Amen.

@2022

WhatsApp Pastor Richard mfate+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.