SOMO: AFYA YA AKILI YAKO.
Shalom Mwana Wa Baba Yangu Nakusalimu Kwa Jina Yesu. Ameen.
Jina langu: Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania.
Makao Makuu Morogoro Veta Dakawa
Karibu katika Ujumbe huu.
πππππππππππππ
Watu Wengi Sana Wameshindwa Kuzilinda AKILI zao katika hatari mbalimbali za kiroho na Mzunguko mzima Wa maisha wanayoishi Wakesahau kutunza Afya za AKILI. Kiufupi AKILI nikiungo kidogo Sana lakini Kikishambuliwa au kikawa na magonjwa hakitamudu kufanya chochote Watu Wengi huwa hili hatulijui kuwa Afya ya Akili yako ni Ufanisi mzuri Wa namna unavyoweza kukabili changamoto mbalimbali.
AKILI Ni Nini..? Akili ni Uwezo Wa Kufikiri Kuitatua na Kukabili changamoto mbalimbali na Kujitsmbua.
Akili ndiyo inayokuwezesha Kuishi na Mazingira mbalimbali na kila Hali unayoipitia.
ππππ
Mathayo 22:37
Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote
πππππππΏππΏππΏ
1 Wakorintho 2:16Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo
Hii Mistari Inahusiana na Akili utaona mwanzilishi Wa Akili ni Bwana pia Sisi Tumepewa Akili za Kristo.
KUNA MAMBO MATANO YANAIPA AFYA AKILI YAKO.
AFYA YA AKILI HUDHIHIRISHWA NA HAYA
1:UWEZO WAKO WA KUFIKIRI:
ππΏππΏππΏππΏππΏππΏππΏππΏSoma huu mstari
2 Wakorintho 8:21
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Hii Huwa Ni Hali ya Kusikia kitu haraka nakukipa tafsiri kinamanisha nini Pasipo kukosea kukitafsiri.
Unaweza Kuona Picha Ya Kitu au Kusoma kupitia Kufikiri ukajua maneno yanakulenga ufanye nini na kwa nini..?
2:UWEZO WAKO WA KUTAMBUA VITU.
ππΏππΏππΏππΏππΏππΏππΏππΏππΏππΏSoma huu mstari
Mithali 1:2
Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu;
Hii Huwa ni Hali ya kuvijua vitu mbalimbali nakuzipa majina kila kitu unachokipitia umekipa jina au Hali Fulani unapitia lakini unaipa jina.
Mfano Mimi naumwa kwanini useme hivyo ni kipindi unachokipitia unakipa jina la hivyo.
Hiki huitwa nguvu ya kutambua kunawatu wenye Afya ya akili iliyolala Hawezi Kuyajua Mazingira na Mazingira yatamsumbua Kisa Uwezo wake wa kutambua upo chini.
3:UWEZO KUTATUA NA KUKABILI VIPINDI MBALI MBALI UNAVYOPITIA.
ππΏππΏππΏππΏππΏππΏSoma mstari huu
2 Wakorintho 10:3
Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
Kutatua Huwa ni Hali Ya Kujipatia Malibu Sahihi na Kuvuka Katika Kipindi unachokuwa Unakipitia Pasipo Kukuletea Madhara ya Kiakili au Kisaikolonji.
4:UWEZO WA MAARIFA WA KUBUNI VITU MBALI MBALI.
ππΏππΏππΏππΏππΏππΏSoma mstari huu
Mithali 1:7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Huwa ipo nguvu ya kuanzisha vitu na kusimamia kile kitu chochote ukiona unakisimamia kitu na Kukifanya Kiendelee Vizuri na Kukupa Matokeo mazuri
Watu wengi wanaanzisha vitu haviendelei Shida ni Akili Inakuwa Imezungukwa na mashambulizi ya kila namna Unajikuta unashindwa kuyapatia majibu.
Maarifa huwa chanzo cha Kufikia hatua unayotaka ufikie hatua uliyojiwekea Kufikia
5:UWEZO WAKO WA WAZO LAKO.
ππΎππΎππΎππΎππΎ✍πΎ✍πΎ✍πΎ
Ayubu 20:2
Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.
Huwa ni Hali Ya Wazo kuja akilini mwako likikuongoza nini ufanye ni Usifanye
Uwezo wa Kutawala Mawazo Mbalimbali Yanayokuja Kukutoa kwenye Kusundi au malengo uliyojiwekea.
Ni uwezo mkubwa wa kusimamia Wazo lako Unaloliona linakupa Matokeo Mazuri.
TUFANYE NINI KUZILINDA AKILI ZETU.
ILi uweze Kuifanya Akili Yako iwe na Afya
Fanya haya ninayoenda kukufundisha.
ππΎππΎππΎππΎππΎSoma huu mstari
Tito 3:3
Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana...
Unapaswa Uvilinde hivi Sana
1:LINDA MAWAZO YAKO.
Usiruhusu Mawazo mabaya au ya Kukata Tamaa Yatawale kwenye Mawazo YAKO.
Adui Huwa Anatumia Mawazo Yako Na Dhambi Huwa inapata nguvu kupitia Wazo. Tengeneza Mawazo Yenye Afya ndani Yako.
Anza kuwaza Mazuri na Yanayokupa ushindi wa maisha Yako mwenyewe.
2:LINDA FIKIRA ZAKO.
Hakikisha Hufikirii Jambo vibaya kila unaloliweka Kwenye Fikira ZAKO linaenda kuupa mwili Ugonjwa wa Akili Kuendeshwa Nakuishi Maisha hayo unayoyafikiria muda mwingi Akili utaipa udhaifu mkubwa isifanye mengine itendee kazi inayofikiria.
JIFUNZE KUYADHIBITI HAYA NILIYOKUANDIKIA UTAIFANYA AKILI YAKO IWE NA AFYA SANA NA ITAKUWA NA UWEZO WA KUKABILIANA NA HALI ZOTE UNAZOZIPITIA.
HITIMISHO
Akili huitaji Kutunzwa na Kulindwa Sana Isivurungwe Isivamiwevamiwe na matatizo ya kisaikolonjia yanayomvamiaga MTU kupitia kufikiri na kuwaza Sana.
Furaha yangu ujumbe huu nimeuleta kwako muda muafaka upone hizo Fikira.
WITO.
Karibu Sana Upate masomo mengi jiunge kwenye Group LA Maombi na Mafundisho+255710889892
Shirikisha watu wengi Sana
Maoni
Chapisha Maoni