VIKUNDI VYA MAOMBI MIKOANI
UTARATIBU WA VIKUNDI VYA MAOMBI KILA MKOA TUTAKAVYOUONGOZA NA KUSIMAMIA SISI VIONGOZI
Tunalenga Kujifunza na Kuomba Bila Kukoma
Kama Neno linavyotuangiza
πππππππ
1 Wathesalonike 5:16-18
[16]Furahini siku zote;
[17]ombeni bila kukoma
[18]shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
πππππππ
Kila mtu ni wajibu kujua kuomba na kujifunza kuomba Nami Kama Askofu mkuu wa makanisa ya Holy Spirit church Tanzania (Moto Wa Yesu yenye Usajili no 21139 )Yenye makao yake makuu Morogoro Wilaya ya Kilosa Kata ya mbigiri Kijiji cha mateteni
Napitisha Tuwe na Vikundi vya Maombi kila Tulipo ili kusaindiana Kiroho na Kujengana Kiimani hii baada ya wengi kuniomba tufanye hivi
UTARATABU UTAKUWA HIVI;
RASMI KUANZA:Mwezi wa Pili Tutaanza rasimi saivi Unachotakiwa waandae wanaopenda maombi kuomba na kujifunza nawewe utakayeanzisha hili hapo ndiye utakuwa kiongozi wa msimamizi wa maombi eneo hilo utakapokuwepo.
JINA LA KIKUNDI; WANAMAOMBI MOTO WA YESU (W.M)
MSTARI UNAOSIMAMISHA KIKUNDI: Soma 2Wakoritho;10;4 Na 1wathelonike;5:17
Hii mistari inasimamisha.
"""""" .......,,,,,"""""""""'xxxxx,,,,,,,,,,,,
TUTAKUTANA; πIJUMAA MUDA SAA;10;00-12:00 Jioni Tunamaliza Tunarudi majumbani
Tunakuwa Tumefunga masaa 12
ENEO KUOMBEA; πTutakuwa na mzunguko wa kuzungukiana Sisi W.M Kila aliye kwrnye kikundi tutamfikia kwake.
SADAKA: πTutakuwa na matoleo kwa ajili ya kikundi chetu kukifanya kiwe hai baadae Tunaweza Tengeneza Matishet yatakayochapwa Jina la kikudi. MSIMAMIZI ATACHANGUA KIONGOZI WA KUTUNZA SADAKA NA KUMBUKUMBU ZA MATUMIZI YATAKAYOSOMWA KWA WANAMAOMBI.
SIFA ZA KIONGOZI WA MAOMBI
ππππππ➖➖➖ππππππ
1;Awe ameokoka na mwenye msimamo wa kiroho asiyeyumbishwa.
2;Awe Anapenda Maombi na mwenye kiu ya maombi
.
3.Awe na upendo kwa wegine na mwaminifu wa kuzingatia muda wakukutana.
4; Awe ndani ya Hili Group la Maombi Hata Kama Patakuwa na Maelekezo kutoka Kwa Mungu Juu ya Kikundi alichonacho apokee.
SIFA ZA MSAINDIZI WAKE ZIFANANE NA SIFA ZA KIONGOZI MSIMAMIZI.
ππππππππππππππ
SIFA ZA MWANAMAOMBI.
ππππ➖➖➖➖ππ➖➖πππ
1.Awe mtunza siri za kikundi chenu na Siri Za Wezake Asienenze Matatizo au wanayopitia wezake nje ya kikundi.
2.Awe mtiifu na mwenye kuheshimu anayemuongoza
3.Akiona maono au ndoto juu ya maombi yao Awaeleze viongozi wake wa maombi nao wakishindwa kuelewa watanipigia Simu nakunieleza.
4:Mwanamaombi atoke dhehebu lolote Imladi anataka kujifunza kuomba na kuombeana.
5:Kila Jumapili ataenda kushiriki nakuabudu kanisani kwake Awe Anakanisa au Dini yake.
6;Awe mwaminifu wa muda na Kujali Maombi
7:Awe mtu mwenye kushirikisha wengine kuja kwenye maombi.
8;Anaweza akawa kwenye group la maombi au asiwemo
NAMNA YA KUENDESHA IBADA.
1:Tutafungua kwa maombi Dakika 5
2;Nyimbo za kusifu na Kuabudu Dakika 10
Mnatoa Sadaka Kabla ya Neno
3;Somo fupi litakoenda dakika 15.
Kila mtu mwenye uwezo wa kufundisha atapangwa.
4:Maombi na Kuombeana.Dakika 30.
.
KUOMBEANA
πππππ
Tutaandika mahitaji yetu 10
Tunakuwa tunaombeana Kila hitaji likijibiwa tunaweka jingine
Kila mmoja atabadilishana ile karatasi na karatasi ya mwezake UNAOMBEA KWA KULITAJA JINA LAKE DAKIKA 20 KISHA
Kila mmoja ataandika Jina lake kufanya urahisi kwa Anayemuombea. KISHA MKIMALIZA KARATASI ATARUNDISHIWA MWENYE NAYO MSICHANE MPAKA UMEJIBIWA UNATIKI KAMA IKICHOKA UNAKOPI NYIGINE MAHITAJI HAYO HAYO.
ππ KUOMBEA ENEOππ
MTAINGIA MAOMBI YA KUOMBEA ENEO MLIPOKUTANIA KUKAMATA ANGA ARIDHI YA MTAA HUO
MTAOMBEA ARIDHI NA HILO ENEO WATU WAZIDI KUJIUNGA NANYI
MTAOMBEA FAMILIA YA MLIPOKUTANIA
MTAOMBEA KAZI ZENU MAHUSIANO YENU NDOA WATOTO WENU
MTAOMBEA ROHO ZINOZOWACHELEWESHA
Kisha mtamuombea Pastor Richard Mwanzilishi wa maono na kuombea uongozi wenu kisha funika kwa Damu ya Yesu Mahitaji yenu
.MWISHO
Fugeni kwa Maombi nakupeana mkono.
Kama kuna matangazo au taarifa imetoka huku juu Mnapeana
MSINGI WA IMANI YETU.
Watu wafundishwe na waweze kujisimamia wao kama Wao Bila Kutengemea mtu.
Mathayo:28;18-20
Usiwaaminishe watu mafuta au chumvi au maji waaminishe Jina la Yesu linanguvu kwao Pia Neno la Mungu Lina nguvu kwao.
Ukisikia Sauti ya Mungu uwe makini na ujihakikishie Ni Sauti ya Mungu Kweli kama hutaelewa Mpingie Pastor Richard unamweleza
.πππππππππππ
JUMAPILI KILA MTU ANAENDA KUABUDU KANISA LAKE IJUMAA TUNAKUTANA.
Nitumie Jina full na mkoa na wilaya kijiji utakapokuwepo na simu yako.
Karibuni Tuanzishe vikundi vya kuomba kwa kushirikiana na wengine.
.Yohana 15:7
[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Luka 11:1
[1]Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
Maoni
Chapisha Maoni