SOMO;NAMNA YA KUIFANYA IMANI ILETE MATOKEO
SOMO: NAMNA YA KUIFANYA IMANI ILETE MATOKEO;
,,,,,,,,,'''''""""""""",,,,,,,,,,,,^^^^^^^^^^
UTANGULIZI;
Naitwa Pastor Richard Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania Moto wa Yesu
Watu wengi Wana Imani Lakini Hawana Imani Yenye Kuwapa Matokeo Ya Kile Wanachokiamini Watu Wengi Huweza Kuomba Vizuri Lakini Imani Ya Kuwapa Wanachokiamini hapo ndipo palipo shinda..
Imani hubembwa na mtu mmoja Anayekuwa anauhitaji wa Kuamini Jambo fulani Akifanya au Akiomba Ataona matokeo
Imani huwa si kubashiri au Kutumaini Kitu Ambacho huna uhakika nacho.
WATU WENGI HUJUA IMANI NI HAKIKA YA MAMBO YATARANJIWAYO
👇👇👇👇👇
Waebrania 11:1
[1]Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
WACHACHE HUJUA IMANI NI UKAKI WA KILE UNACHOKISIKIA AU KUKITAMKA SAWA NA ANDIKO HILI
👇👇👇👇🌴🌴🌴🌴🌴
Warumi 10:17
[17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Kwa Lugha rahisi Anamanisha huwezi ukawa na imani kama huna Neno yaani mafundisho ya Neno la Mungu. Imani hujengeka kupitia unapoona Kusikia na Kutenda Jambo.
KAMA UTAKUWA WA KUSIKIA
1.Hatia ndani yako ujue utakuwa hivyo hata kama ulishakombolewa.
2.Kama utasikia wewe huwezi Kuolewa au Kudumu kwenye uchumba Imani itajengeka hivyo.
3.Kama Utasikia magonjwa ndani Ya Mwili Utayafanya magonjwa yasiishe ndani yako
Inatengemea Unasikia nini
MAMBO YA KUZINGATIA KUONGEZA IMANI YAKO.
1.Omba Jifunze Kuomba Imani itaongezeka.
2.Upate Baba wa Kiroho Anayefundisha Siyo anayehubiri.
3.Watu waliojikatia Tamaa au Wasio Na Imani Waache Tafuta watu Wasiojikatia Tamaa.
4;Uwe mvumilivu na mwenye subira huku ukilelewa katika Madhabahu Sahihi.
5:Uwe mtoaji Kwa Mungu na Mwenye Kupenda Kujifunza Siyo Kuombewa.
HATUA ZA KUIFANYA IMANI IKUPE MATOKEO.
1:ANZA NA KUONGEA UNAVYOTAKA IWE.
Soma
👇👇👇👇🖊
Luka 18:38
[38]Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.
Hapa Tunaona Huyu Batharamayo Kipofu Anaongea Anaomba Lazima Umuite Yesu Haijarishi nyakati unazopitia Imani huwa haizamishwi na mapito au changamoto.
Huyu kipofu walikuwepo wengi waliomuita Yesu lakini Hakuchoka kuita.
Imani huwa haichoki mpaka imepata kile ilichoitaji hiyo ndiyo sifa ya Imani.
2:KUWA NA UHAKIKA ULICHOSEMA MWENYEWE
Soma👇👇👇
Luka 18:41
[41]Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona.
Hatua Ya Pili Imani uwe na Uhakika wa unachokiongea mwenyewe.
Huyu Kipofu Anasema Anataka Kuona hakuwa na maneno mengi hakutaka Ajieleze kwa Yesu Watu wengi Imani zetu zinafeli hapo kwenye manug,uniko, kujieleza,
.mfano umeulizwa unataka Mungu akufanyie nini
Mtu anaanza natamani mwaka huu niolewe harafu nijenge nimlipie mwanangu Ada nadhiri yangu niitengue Kumbe jibu ilikuwa niolewe au mwaka huu niowe.
Jifunze kitu kwa imani ya huyu kipofu.
3:FANYIA MAAMUZI ULICHOKIONGEA.
Kama kinaitaji uombe Anza Kukiombea
Kama kinaitaji Pesa Anza Kutafuta Pesa.
Onesha Jitihada Imani hutenda Palipo na matendo
👇👇👇Soma
Yakobo 2:20
[20]Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
KIPOFU ALITEMBEA AKAMFIKIA YESU HATA YULE MWANAMKE ALIFANYA KITENDO IMANI UKIWA UNAONGEA BILA MATENDO KUJISHUGHULISHA JUU YA ULICHOSEMA HAIWEZI KUKULETEA MAJIBU
SOMA VITABU HIVI: LUKA:8:40-56 1wafalme.18;20-40 Luka.8;35-44 Tafakari ujifunze imani.
Acha kuwa muongeaji usiyeweka jitihada Juu ya ulichokisema kwa imani.
4:,AMINI IMETENDEKA.
Yule Kipofu aliamini Kupitia Kumuita Yesu upofu utatoweka nitapona
Luka:18;35-44
ELIA Aliamini Akimtolea Sadaka na Kumjenga Madhabahu Mungu itamfanya Atakapomuita Ajibu maombi yake
1wafalme;18;20-40
Mwanamke Aliamini Kuwa Akigusa Pindo Ataponywa Damu itaacha Kumtoka
Luka:8:40-45
Lazima Uamini mwenyewe mwenye Tatizo Siyo mchungaji bali wewe.
Kwa Shuhuda hizi za kwenye Biblia Unaona Walimfata Yesu Wakiwa na Imani ndivyo unavyotakiwa imani yako iongoze ianze Kukupa matokeo.
Hali yoyote inayokutesa kwa kuwa fikira zako zimeamini nakuruhusu lakini Badili sasa uamini umeponywa.
HITIMISHO
Watu wengi imani zao wamewategemea watu hawataki Kujifunza au kulitafuta Neno la Kristo na mwisho wao wamekuwa wakitiwa mioyo kwa kuabiwa pokea pesa pokea majumba pokea gari nao wanaitikia Amen wanabaki wakigonja kumbe wagepata masomo yagewapa ufahamu wa kufanya kazi kupitia Jitihada zao Mungu Angewabariki.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
KUTOKA KANISA LA HOLY SPIRIT CHURCH TANZANIA MOTO WA YESU.
IFANYE IMANI YAKO IKUPE HAJA YAKO
Shirikisha wengine Somo hili.
Maoni
Chapisha Maoni