SOMO:MAOMBI YA MWISHO WA MWEZI NA MWANZO WA MWEZI
SOMO:MAOMBI YA MWISHO WA MWEZI NA MWANZO WA MWEZI.
🍀🍀🍀🍀🍀🍀🍀🍀🍀🍀🖍🖍🖍🖍
Wakati nafunga mwaka nikiwa katika kuwaombea mahitaji mliokuwa mmeyatuma nikiuganisha na ya kanisani maelekezo yaliyotoka katika kuwaongoza watu mliopo kwenye Group kutoka kwa Mungu mwenyewe Akasema mtakuwa na maombi ya mwazo WA MWEZI na Mwisho wa Mwezi yatakayokuwa yanaombwa mwisho wa mwezi maelekezo ya uombaji yalikuwa kama ifatavyo;
Mungu wetu hutembea katika maelekezo hapa Yoshua anapata nguvu kusimamisha mwezi hata wewe mwezi ukakutii ukalete Baraka zako upokee ushuhuda kila mwezi
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
👇👇👇👇👇
Yoshua 10:12-13
[12]Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli,
Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni;
Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
[13]Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia,
Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao.
Hayo, je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima.
Soma👇👇👇👇
Kutoka 40:2
[2]Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.
🖊🖊🖊🖊🖊✅✅✅✅🖊🖊🖊🖊🌴🌴🌴
TAFADHALI SOMA MAELEKEZO UYAELEWE TUTAKAVYOOMBA
1:Kila mtu ataandika mahitaji 10 anayotaka Mungu Amtendee kupitia hii madhabahu ya Holy Spirit church (Moto wa Yesu) ndani ya huo mwezi..
Mfano Tar 30/1/2024 Jina; Richard Julius Kushoka
MAHITAJI YANGU
Nataka Mungu kwa mwezi huu ninaouanza akanitendee yafatayo kupitia madhabahu hii ya moto wa Yesu
1.Nipate kazi serikalini
2 Huduma Yangu izidi kusitawi
3.Nipate watoto siyo mtoto
4 .Nilipwe madai ninaowadai
5:Nikapate mke sahihi wa kuowa
6;Nipate Kiwanja nijenge
7:Nipate visa ya kwenda marekani.
8;Nyumba yetu tuimalize
9;Mke wangu apate kibali kila aendapo.
10;Nikue na kuongezeka kiroho.
Ninaomba Eeh Bwana Yesu mahitaji haya ukayatende ndani ya mwezi huu ninaomba yapokee katika Jina la Yesu.Amen
Kisha endelea kuomba mwenyewe
➖Utayaombea kila Wiki yaani siku ya 7 kila siku ya 7 ndani ya huo mwezi unakuwa unahesabu siku 7 unayaombea.
➖Muda Wowote na sasa yoyote iwe usiku au mchana inatengemea muda wako
➖Kama utakuwa na Sadaka unayotolea kama huna unaomba tu haya maombi yapo huru utoe Sadaka au usiyatolee.
➖Kila Hitaji litakalojibiwa unaondoa unaweka ligine tena hakikisha yanatimia maombi kumi.
2:Kila mwezi unapofikia mwisho wa mwezi utanitumia mahitaji yako mimi Baba yako wa Kiroho Kama Mungu atasema nawewe atakuletea ndoto au maono au sauti uniambie mimi baba yako wa kiroho .
➖Ukishayatuma WhatsApp kwenye inbox yangu unaniambia nayasoma kisha nitakujulisha upinge au unaweza ukapinga simu nakuombea pamoja na mahitaji hayo kumi.
3:Maombi haya yanawalenga waliopo kwenye group la maombi siyo aliye nje ya group haitakiwi umuombee mahitaji ya mtu mwingine unatakiwa uombee mahitaji yako.
4:Tutakuwa Tar 30 na 31 inatengemea mwezi unaishia Tar ngani.
TUTAOMBA KUOMBEA KUMALIZA MWEZI SALAMA 2024
.
OMBA HIVI.
Nashukuru Sana Bwana Wangu umenivusha tena huu mwezi mimi ninakushukuru Sana naomba ukaubariki na uutawale mwizi wa ___2 Ninaoenda kuuanza naukabidhi mikononi mwako nakataa roho za magonjwa roho za kushindwa roho za kuteseka tena ninazifunga zisipate nguvu kuniendesha mwezi ninaouanza tenda Bwana Kwa Ajili ya utukufu wako katika jina la Yesu. AMEN
KISHA ENDELEA KUOMBA KADIRI MANENO YANAVYOKUJA KWAKO.
5:Kishamaliza omba kukataa roho za visasi au mashambulizi kwako mwezi mzima kataa.
Nakataa roho za visasi roho za mashambulizi roho zakunishusha kimaombi na kiroho ninazikataa katika Jina la Yesu.Amen
Tutaomba hivyo
Kisha Soma hivi vitabu
👇👇👇👈👈
Isaya 60:20
[20]Jua lako halitashuka tena,
Wala mwezi wako hautajitenga;
Kwa kuwa BWANA mwenyewe atakuwa nuru yako ya milele;
Na siku za kuomboleza kwako zitakoma.
👇👇👇👇👇
Marko 13:24
[24]Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake.
Jifunze kuombea mwezi maana umebemba mwanga nuru yako mwezi unapouanza uanze na nuru usianze mwezi unakuwa huelewi unaishaje.
Pia hakikisha unafata ulivyoelekezwa kuomba kama hujaelewa nifate inbox unaniuliza.
Share na kuendelea kuwauga wegine
Maoni
Chapisha Maoni