DALILI ZA MTU KUFUNGULIWA ANAPOOMBA
SOMO: DALILI ZA MTU KUFUNGULIWA ANAPOOMBA.
Tunapoomba huwa hakika ufalme wa ngiza tunaupiga na kuubomoa huwa Ni vita kwa sababu ule ufalme wa ngiza unakuwa ulishazoea kumtesa mtu na kumfunga na watu wanateswa na majeshi mengi mfano. Mtu unamkuta Anakuwa anahofu, Anakata tamaa,Ananug,unika,Anahasira, Mwoga anahirisha ahirisha vitu hili huwa jeshi la mapepo katika ufalme wa ngiza. Mwigine Anateseka na magonjwa yasiyoeleweka, Vitu vyake vinakufa kufa tu, Anashika mimba zinaharibika, Hashemi mimba au uume hausimami, Anasikia vitu sehemu za siri, kutokwa blidi isiyoisha, au kukosa blid nk. Hizi Dalili za Jeshi la Wachawi na Waganga Mwigine Atakuwa Anaota ndoto watu waliokufa anaongea nao, au anaota yupo makaburi,au misimba au yupo kijijini alikosomea,au kuota wamasai au wanyama kama ng,ombe nk Hili ni jeshi la mizimu
Mtu mmoja unaweza Kumkuta anateseka na haya majeshi yote Wachawi wanamtesa Mapepo na mizimu huyu mtu anapokuja kuanza kujifunza kuomba na akaelewa kuomba kwanza anakuwafire Anaanza kuomba kila anapoomba ufalme wa Jeshi fulani anaupindua kila atakapoomba falme zote hataziondoa kwa maombi ya siku moja kama watu wanavyofikiriaga Kuwa rahisi rahisi ukianza kuomba unaviamsha hata vilivyojificha ndani mwako maana vinakuwa vinaugua moto ndani ya mwili ulipokuwa huombi vilikuwa haviuugui na vinajua wewe vitakutesa.
SOMA HUU MSTARI
👇👇👇👇👇👇👇
Waefeso 6:12
[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Vita yetu tunapoomba ipo kiroho tunaupindua ufalme uliotesa maisha yetu kwa hiyo hebu uwe Siriazi kufata ninavyokuongoza kuomba na kupambana katika maombi pia acha kujidharau kuwa huwezi kuomba wakati maombi yanakuwa yameandikwa. Kumbuka hii nakusaindia wewe mwenyewe faida ni yako mwenyewe Na usipopenda maombi hizi falme zitakutesa tu sababu umezipa uhuru zikuendeshe.
Dalili zifatazo hudhihirika mateso yanapoondoka mwilini mwako unapoomba.
👇👇👇👇🌴🌴🌴🌴🌴🖊🖊🖊🖊
1;Utaanza kuona kuishiwa nguvu na wakati mwigine kudodoka chini usishagae unafunguliwa.
2:Utaanza kuharisha na kuumwa tumbo kama linavuruga Usishangae unafunguliwa.
3:Utaanza Kutema mate na kuhisi kichefu chefu na wakati mwigine kutapika
4:Utapiga miayo mifufulizo na mingi sana.
5:Ndoto utaanza kuota ndoto nzuri siyo za kutisha.
6:Utahisi vitu vinatoka kwenye sehemu za siri saa nyigine utaviona kwa macho saa nyigine utahisi tu hutaviona.
7:Machozi kutoka nakulia bila sababu
8;Utaona nguvu ya kuomba tena kuongezeka hamu ya kuomba unatamani kila saa uombe.
9:Utaanza Kupenda Maombi Kupenda Kutoa Sadaka Kupenda injili iwafikie wegine utapenda watu waokoke utatamani wamjue Mungu hii hali hutokea unapofunguliwa
10;Utaanza Kujiona unahuduma utatamani ukafungue kanisa au uanze kumtumikia Mungu Kwa nguvu zote.
11: Wapo watu hutapika damu vitu mbalimbali .
12;Utaanza Kuona Mwili unaanza kuwa mwepesi na kutamani kukifanya ulichokuwa huwezi kukifanya.
Tusome maandiko haya.
HAPA YESU ANATUANGIZA TUWE TUNAOMBA SIYO TUKAOMBEWE KILA MMOJA AKIFUNDISHWA KUOMBA ATAJUA
👇👇👇👇👇👇👇👇
Luka 11:9-10
[9]Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
[10]Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
MUNGU ANASEMA NA WALE HUOMBA KINDOGO TU ANAACHA ANABAKI ANASUBIRI ALICHOOMBA
👇👇👇👇👇👇👇
Yohana 16:24
[24]Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Jifunze kitu ufalme wa ngiza haulage au kutulia kwa sababu wewe umeukimbia kwa hiyo unapambana kukurundisha nyuma Simama uwe na msimamo na Yesu Wako usirundi nyuma au kupowa ukawa baridi Biblia inasema hivi:
👇👇👇👇👇👇👇
Ufunuo wa Yohana 3:16
[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
Naitwa Pastor Richard Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania (H.S.C.T) Moto wa Yesu Tupo Morogoro wilaya ya Kilosa Kata Ya Mbigiri Kijiji cha Mateteni.
Nakushauri uwe moto usipende ubaridi wa kiroho Mungu hatembei na watu wasiopenda kujifunza na wasiopenda kuomba jitaidi kufanya mazoezi ya kuomba mara kwa mara maombi ninayokuwa napost.
Kama unakuwa hujaelewa unanifata inbox unaniuliza usiombe maombi kama hujayaelewa.
Maoni
Chapisha Maoni