SOMO:ROHO MTAKATIFU

SOMO: ROHO MTAKATIFU 

Roho Mtakatifu Ni Nani..?

Ni mshirika wa tatu wa Uungu unaowakilisha Nafsi Ya Mungu. Yeye ni Sawa na Mungu Baba Yeye ni Msaindizi wako katika maisha yako ya Wokovu.

Roho Mtakatifu Siyo Nafsi Tu ni Nafsi ya Ki Mungu. Huitwa Mungu mwenyewe. 

     Karibu Somo hili
Linaletwa na Pastor Richard Kwa Msaanda Wa Roho Mtakatifu. Nipo Morogoro Veta Dakawa  WhatsApp +255759861768.

A.ROHO MTAKATIFU ANAZO SIFA AMBAZO NI MUNGU PEKEE NDIYO MWENYE SIFA HIZO.

1.Ana Sifa ya Umilele Hafi Wala Hazikwi.

Ebrania;9:14 Soma.

2.Ana Sifa ya Kuwa Kila Mahali Kwa Wakati Mmoja Dakika Moja Anaweza akawa Arusha Dar Na Zanzibar Kwa muda mmoja akihudumia watu.

Zaburi:139:7-10 soma

3.Ana Sifa Ya Kufahamu Yote Hadi mawazo Yetu Nia Zetu

1Koritho:2:10-11 Soma 

4.Anaweza Yote. Kila Kitu Anaweza Kukifanya chochote kile.

Luka:1:35 Soma

5; Hushirikishwa Majukumu Sawa na Baba na Mwana Katika Utendaji Kazi.

Mathayo;28:19 Soma

6.Alishiriki Katika Mpango wa Ukombozi wa Mwanadamu 

Yohana.16:8 Soma

B.Roho Mtakatifu ni Nafsi.
Wakristo wengi akilini mwao huelewa Roho Mtakatifu ni Nguvu fulani au Ushawishi wa kufanya jambo fulani.Humchukulia Kama Nguvu ya umeme.

Hii Dhana Haipo Kweli Roho Mtakatifu ni Nafsi Hai Yenye Uwezo na mamlaka makubwa.
Yohana:16:13-14 Yohana. 15:26

A.ANAZO SIFA MUHIMU AMBAZO NAFSI ANAZO.
1:Akili =Uwezo wa Kufikiri na Kutenda Jambo

2:Wepesi WA Kuona Kitu= Uwezo wa Kuhisi Vitu vizuri na vibaya kisha kupambana vitu .

3:Utashi=  Uwezo wa Kuchangua Kuamua vitu vya kufanya ambavyo hafai afanye Yeye.

B.UDHIHIRISHO WA NAFSI YAKE.
Waefeso:4:30 Matendo;5;1-4

1:Anaweza Kuona Moyoni mwetu.

Efeso:4:30

2;Anaweza Kufariji unapokuwa na huzuni.

Matendo:9:31 

3:Anaweza Kufikiri Juu Yetu ndani yetu.
Warumi:8;6

4:Anaweza Kuongea Nasisi ndani yetu.
Matendo:13:2

5.Anaweza Kuomba Ndani Yetu.
Warumi;8;26

6:Anaweza Kufundisha maishani mwetu.
Yohana.14:26

7;Anaweza Kuonyesha mambo ya kufanya na yasiyofaa kufanya kama mtoto wa Mungu.

1Wakoritho.12:11

8;Anaweza Kutuzuia Tusifanye vitu vimchukizavyo Mungu.
Matendo;16;6

9:Anaweza Kutenda Miujiza mbalimbali 
Matendo;19;6

Hizi ndiyo sifa zinazomjulisha Roho Mtakatifu ni nafsi hai yenye nguvu na mamlaka.

Roho Mtakatifu kipindi hiki tulichonacho ni kipindi chake ambaye amechukua nafasi kutoka kwa mwana ambeye ni Yesu.
Yeye ni Msaindizi wetu hakuna mwigine.
Yohana:14:16 Soma

C.KUMWAGWA KWA ROHO KULITABIRIWA.

Tunaona Angano la Kale Roho Alikuwa akikaa ndani ya watu fulani fulani ilikuwa kazi kushirikiana naye 
Isaya:61:1-4 Soma

Utabiri wa Roho Mtakatifu kwa Agano la kale manabii walitabiri

1:Roho Wake Angekuwa Ndani ya Juu Ya watu wake Wote
.
Yoeli:2:28-29   Isaya 44:3


2:Mungu Aliahidi Masihi Angejazwa na Kutiwa Nguvu na Roho Mtakatifu.

Isaya:42:1 Isaya.61:1


3.Maneno Kadhaa Yanayodhibitisha UTIMILIFU WA ROHO MTAKATIFU. 

a,Kupokea Roho Mtakatifu na Vipawa vyake.
 Yohana.7:39 Matendo.2:38 Matendo.10:47

b.Kupakwa Mafuta na Roho Mtakatifu 
Kutoka:28:41, 29:29 Zaburi.2:2

c.Kujazwa na Roho Mtakatifu 
Waefeso:5;18 Matendo.2;4b

d.Kubatizwa kwa Roho.
Mathayo:3:11 Luka 3:16 Yohana.1:33

e.Kufunguliwa Kwa Roho.
2Wakoritho.3:17 Yohana. 7:38 

D.UBATIZO KWA ROHO MTAKATIFU 

1:Ushahindi Na Udhihirisho wa ubatizo wa Roho Mtakatifu. 

a.Dalili Za Mwanzo
Ni kuonyesha kwamba umekutana na mabadiliko ndani yako baada ya kuokoka.

b.Dalili ya Ki Maandiko.
Kusoma Maandiko na kuyaelewa na kuwasilisha kufafanua katika kiwango cha Kueleweka.

c.Uzoefu WA Ki Biblia.
Ni utakaso na Kuchukia Dhambi na Kukataa kuishi maisha yanayokatazwa na Biblia.

2:TAARIFA ZA MAANDIKO JUU YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU. 

Chanzo kikuu cha huu ubatizo ni matendo ya mitume ambako kuna matokeo matano yaliandikwa.

a.SIKU YA PENTEKOSTE 
Matendo:2;1-14
Hii ni Taarifa Muhimu yenye utimilifu tuliyonayo.

MAMBO HAYA YALITOKEA SIKU HIYO
1:Upepo Kutoka Mbinguni. 
Siku hiyo ilikuwako uvumi kama upepo mkali.

2:Ndimi Za Moto.
Kulikuwa na cheche za moto siku hiyo.

3.Kunena Kwa Lugha Nyingine.
Mitume waliongea Lugha yake kila mmoja.

b.Nyumbani Kwake Kornelio
Matendo:10;44-48

Petro anasema nilikuja tu kwa kuwa Roho alisema nije kwenye nyumba hii
Matendo:11:12

Petro alianza kuwaeleza kuhusu Yesu
Matendo10:34-43

Maneno mengine Roho alisema ndani ya Petro hivi nani atakayekataza maji watu wasibatizwe
Matendo:10;47

c.Petro Akiwa Efeso
Matendo:19:1-7
Hapa ninaushahindi WA Aina Tatu Petro wakati Anapeleka injili ya umisheni.
1.Watu walinena Kwa Lugha
2:Watu Walibatizwa Katika Roho Mtakatifu 
3.Kupokea Roho Mtakatifu.

d.Uamsho WA injili  Samaria 
Matendo 8 Sura yote Soma.
1.Kulikuwa na Mwitikio mkubwa kwa mahubiri ya Filipo Ambao matokeo yake.
Kulikuwa na mkutano mkubwa wa injili
Na kusikiliza habari za Yesu.
Matendo;8;6


e.Sauli WA Tarso.
Matendo 9 Sura yote.
Tunamuona Sauli anakutana na Kibano cha Roho Mtakatifu Jeuri zake na Matendo yake ya kuuwa wa Kristo iliisha  Soma habari hii


E  ●SOMO: ROHO MTAKATIFU NA MWAMINI.

Katika maisha ya wokovu Roho Mtakatifu huwa kiungo mhimu wa kuyafanya maisha yetu kuwa na Wokovu uliosimama katika Kweli na Kufanya Tuwe watu tunaoishi maisha matakatifu yenye kumpendeza Mungu.

Karibu somo hili:
Naitwa Pastor Richard 
Nipo Morogoro wilaya ya Kilosa Kata Ya Mbigiri Kijiji cha Mateteni 

Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 

Mwamini ni mtu aliyempokea kristo kuwa mwokozi wake wa maisha.

Roho Mtakatifu ni Msaindizi wetu na Ni nafsi ya Tatu ya Mungu Baba.

👉Roho Mtakatifu Humsaindia Mwamini 
Kupata Wokovu kuzaliwa kwa mara ya pili na kuanza kuyaishi maisha ya Kiroho ni Kazi Ya Kwanza Ya Roho Mtakatifu anaomsaada mkubwa kwa mtu aliyeokoka

HAYA NI MSAADA WA ROHO MTAKATIFU KWA MTU ALIYEOKOKA

1.Katuleta Kwenye Wokovu.
Bila Roho Mtakatifu Tusingekaa kwenye Wokovu.

a.Hutupa macho tuone makosa yetu na Tumrundie Mungu.
Yohana.16:8-11

b.Hutufanya Tuokoke na Tubatizwe 
Tunapookoka tunakubali kufata na kuishi maisha ya KiMungu Kwa Msaanda Wa Roho Mtakatifu 
Tito;3:5 Waefeso:2:1

c.Hutuweka Huru na nguvu za dhambi na mauti ili Tuweze Kuwa Watakatifu.
Warumi;8:2

d.Hutupa Uhakika ndani Yetu Kuwa ni Waokovu.
Warumi:8;16, 1Yohana.5;9 


2:Hutupatia Nguvu Ya Kuishi Maisha Matakatifu 

a.Hutuongoza Kwenye Kweli.
Yohana.16:13 

b.Hutufundisha Mambo Yote.
Yohana.14:26

c.Huihuisha Miili Yetu
Warumi.8:11

d.Hutupa Nguvu Kwa Ajili Ya Huduma.
Matendo.1:8

e.Huwekea Maombi Yetu nguvu.
Yuda.1:20 Waefeso. 6:18 

f.Husukumiza Sifa Na Ibada Kwa Mungu.
Matendo.2:11 Waefeso;5;18-19 Wafilipi. 3;3

g.Hutupa Tunda la Roho Mtakatifu Katika Maisha ya Mwamini
Galatia:5:22-23 


B.KUPOKEA ROHO MTAKATIFU. 

Kuna hatua za kufata unapotaka Kumpokea Roho Mtakatifu 
Ambazo ni hizi zifatazo.

1;Lazima Uokoke Umpokee Kristo Kama Mwokozi Wako.
 Ni vyema umkiri Yesu na umpokee awe Bwana Kwako na Mwokozi Wako.

2.Lazima Uitake Baraka hii.
Uwe na Kiu mwenyewe  
Yohana.7:37

3.Maneno Manne Unayotakiwa Uyajue.

a.KATAA; Paulo aliwaambia waliokoka kuwa tumeamua kukataa mambo yatakayotupa aibu.
2Wakoritho:4:2

b.TULIA;Unatakiwa uache hofu au wasiwasi tulia Uone mkono wenye nguvu.
Tulia kiakili Tulia Kimwili Tulia .
Matendo:2:2

c.POKEA; Ni vyema umuombe Yesu akubatize kwa Roho 
Luka:11:13
Muombe kwa utaratibu kiurahisi na Kwa Imani
Utakapoomba Amini Umejibiwa.

d.ITIKIA. unatakiwa uwe na mwitikio nguvu ya kukusukuma kuomba mwenye nguvu ya kuyaendesha mambo kiroho.
Matendo:2:4


C.KWANINI TUNENA KWA LUGHA..?

Hii ndiyo utimilifu wa mkristo kunena kwa Lugha mpya.

1;Ushahindi wa Ki maandiko wa ubatizo wa Roho Mtakatifu 
Ukisoma Matendo:2:4

2.Ni Mapenzi Ya Mungu Kwa Ajili Yetu.
Mungu anasema kupitia Paulo Nami nataka ninyi nyote mnene Kwa Lugha.
1Wakoritho:14:5

UWEZO wa Kusema Kwa Lugha hutolewa na Mungu tu kupitia Roho Wake.

3.Namna Ya Kuponywa na Kutakaswa na Kuwekwa Huru.
Warumi:8;26
Neno linatuambia moja ya udhaifu wetu sisi hatujui kuomba ipasavyo.

Mfanywe wapya nia zenu katika roho
Waefeso:4;23


4;Ni chanzo za Kujijenga Binafsi.
Yeye annealed Kwa Lugha Hujijenga Binafsi
IWakoritho:14:4

5.Ni Eneo la Ushirika WA Kiroho WA Kweli na Mungu.
Maana anenenaye Kwa Lugha hasemi na Watu Bali husema na Mungu mwenyewe 
1Wakoritho:14:2 1Koritho. 2 Sura yote.

6.Hutuweka Tumkubuke Roho Mtakatifu aliye ndani Yetu.


7.Hutusaindia Kujifunza Kuishi Kwa Kumtengemea Mungu.
1Wakoritho.14:6

8:Kufunguliwa Kwa nia sahihi za moyo.

9:Ni Nafasi Ya Kutoa Shukurani Kwa Mungu Kwa Namna Alivyotubadilisha.
Yohana;4:24

10;Humwezesha Mtu Kuomba.
Nitaomba Kwa roho nitaomba kwa akili 
1Wakoritho. 14:15
Warumi;8;26-27

11:Ni Chanzo cha Raha na Furaha.
Isaya:28:11-12

12;Ni Huduma Ya Sifa na Ibada Kwa Mungu.
Matendo;10:46, 2:11

13:Hutupa nyimbo na Namna Ya Kuimba katika Roho Mtakatifu 
Wakolosai:3:16 Waefeso:5;19

14:Ni Namna Ya Kiroho ya Kudumisha utimilifu wa Roho 
Waefeso:5:18-19

15:Huwajenga Wengine Kupitia Kunena kwa Lugha.
1WAKORITHO.14:5

16;Ni Ufunguo Wa Kuleta Nia Zetu Kuwa Za Kikristo.
Yakobo:1:26, 3:1 Waefeso.4;29


D.(i).KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU.

Karama za Roho Mtakatifu ni uamusho wa Kikarisma. Huu ni uamusho wa Kiroho unaofanyika ndani ya maisha ya mwamini. Karne 50 zilizopita Roho alikuwa hakuna ilikuwa hali ya ukame miaka 20 iliyopita uamsho huu unakuja kwa Kasi Zaidi makanisani.
Tusome 1WAKORITHO:12:1

1;AINA ZA KARAMA 
Zipo Karama nyingi Za Kikarisma Zilizotajwa Katika Biblia
Rejea na Usome; Warumi.12:1-8 Waefeso.4:11

Kurahusisha Kusoma Makundi hayo nitayaweka Sehemu kuu Tatu.

A.Karama Za Kusema.
Hizi ni Karama za Kusema 
1:Lugha,; Kuongea Lugha Nyingine 

2:Kutafisiri Lugha: Kuelezea wengine lugha iliyongeni masikioni mwao.(Mkalimani)

3:Unabii: Kutamka yajayo na yaliyopo au yaliyopita

B.Karama Za Ufunuo.
Hizi ni Karama za ufunuo 

1.Neno la Hekima. Ni mtu kuwa na Hekima kufanya mambo yanayoeleweka.

2.Neno la Maarifa. NI mtu kuwa mbunifu na mwenye kufanya vitu vya tofauti na vyenye kuingwa na Jamii.

3.Kupambanua Roho; Kuzitofautisha roho za shetani na Mungu.


C.Karama Za Uwezo.
Hizi ni Karama Za Uwezo.
1.Karama Ya Imani.
Hii ni Karama inayomuongoza mtu kuitawala hisia zake na fikira.

2.Karama Ya Uponyaji.
Hii inamfanya mtu awe na uwezo wa kuponya watu.

3.Matendo na Miujiza.
Humfanya mtu atende miujiza mingi nakutenda kwake kufungua watu.

🍇🍇🍇👇👇👇👇
(ii.)ROHO MTAKATIFU ANAWEZA KUMTUMIA NANI  KARAMA HIZO.

a.Mshirika Yeyote Anaweza Kutumiwa.
1WAKORITHO 12:7-11,   14:26:31

b.Tunabidi Tujazwe Roho (Waefeso.5:18

c.Lazima Tutake Sana Karama zilizo Kuu.
1Wakoritho:12:31

d.Tusikose Kufahamu Kuhusu utendaji wake Karama
1Wakoritho 12:1

e.Inabidi Tuwe na Hamu Kiu ya Kupata Karama za Roho Mtakatifu. 1Wakoritho:14:1-6)

f.Inabidi tupate upendo na kutiwa motisha na wapendwa wezetu 1Wakoritho 13 Sura yote


3. KARAMA YA LUGHA. 

a.Inafanya shughuli mbili kwenye maisha ya mwamini nazo nizifatazo.

1:Kwanza: Humjenga Kiroho na Kumfundisha mtu anayeiongea lugha hii.

2:PILI; Hujenga Kanisa na Watu wengine wanaposikia lugha hii.


b.MTIRIRIKO WA KUTUMIA LUGHA KWA WATU WENGI MHADHARA.

1.Maneno uyatoe yenye Upendo Uso wako onesha furaha uso wa Upendo.
1Wakoritho. 13:1

2.Inabidi uendane na mazingira na ufatane na tafsiri usichanganyechanganye.
1Wakoritho:14:5

3.Kama itatokea Roho Mtakatifu ameshuka mnene wawili au watatu tena kwa kupeana mwanya nafasi.
1Wakoritho.14:27

4.Kufasiri Lugha (1Wakoritho.12:10)
Hii hutokea mtu mmoja ananena mwingine anafasiri hili huwa tukio la Ki Mungu. 

Nani anaweza kuitumia hii ni mtu yeyote Roho Mtakatifu Anaweza Kumtumia
1Wakoritho.12:11


5:KARAMA ZA UNABII.( 1Wakoritho.12:10)
Neno Na Nabii linamaana Useme maneno yaliyovuviwa na Roho Mtakatifu 
Soma 1Wakoritho.14:31

a.Kusundi lake.
Usemi wa Kinabii kama huo ni-:

1.Kujenga.
Hii inamaana ya kujenga kuwatia waamini nguvu ya kuwaimarisha kiimani.

2.Kufariji. kusema maneno ya faraja.

3.Kutia Moyo.kuchochea na kuwaamsha waamini.


b.Aina Tatu za kuchanganya kuhusu unabii.

1.Isichanganywe na Kuhubiri.
Watu wengi leo karama hii wanaitumia kuhubiri baadala ya kusema tu.


2.Karama ya Unabii si kwa ajili ya kuhubiri mambo yatakayotokea Hii Karama ni Ya Kusema Wazi Wazi siyo kuhubiri.
1Wakoritho.14:3

3.Karama hii si ya watu binafsi wanaocheza na akili za watu hii ipo wazi karama inaweza kuwa kwa kila muamini
Yakobo:1:5


c.Mafundisho Ya Ki-Maandiko Juu Ya Karama Ya Unabii.

1.Unabii ni Uwezo Wa Kunena na Watu kwa nguvu za Mungu 
1Wakoritho 14:3

2.Unabii hauitaji Kufasiriwa unakuja wazi kwa lugha ya mahali husika mtoa unabii alipo.

3.Unabii Humsandikisha Mjinga.
1Wakoritho.14:15-16

@Ataamishwa Juu ya mambo ya Mungu.

@.Moyo wake utapimwa kwa Yote

@.Siri zake zitafichuliwa

@.Ataanguka mbele za Mungu Kwa Unyenyekevu.

@Atakubali kweli Mungu Yupo katikati Yetu.

@Atamwabudu Mungu na Hatamuacha.

4:Unabii Hutenda Ili Watu Walioamini waweze Kujifunza 
1Wakoritho 14:31

5.Unabii Kila Mtu anafaa awe nayo.
1Wakoritho. 14:1,39

6.Mtu Anayetumika Kwa hii ya Unabii Anahusika kwa matumizi ya maneno mabaya au mazuri.
1Wakoritho.14:32


7.Kwa Sababu Wale Ambao hutoa Unabii Wanaweza fanya dhambi basi unabii lazima Upimwe.
Yeremia:14:14-15,23:30 Kumb.Torati.18:20-22


8;MUONGOZO WA KUPIMA UNABII

a.Nabii anatakiwa asichukie au kulipiga Neno linalomtaka kila Neno kabla hajalisema alipime kwanza limetoka Kwa Mungu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.