SOMO;MAOMBI YA KUOMBA MUNGU ATIMIZE NENO LAKE KWAKO


SOMI;MAOMBI YA KUOMBA MUNGU ATIMIZE AHADI ZAKO KWAKO ALIZOKUAHIDIA

Karibu;
Kuna wakati Mungu anaweza Sema nawewe atakufanyia kitu au nyumba yako au watoto wako au ndugu zako na ukasimama katika maangizo yake vizuri kabisa kama Ibrahimu cha ajabu muda ukazidi kwenda Hajibu Unachotakiwa Usiache kuendelea kuwa mwaminifu kwake na kufata alichokuagiza lakini utaingia kumkumbusha ahadi yake.

Zipo ahadi zetu huibiwa na Adui  kwa kupitia dhambi au kumuasi Mungu au kuto tii maagizo yake.
Mwadaaji wa Maombi haya Pastor Richard Kwa muongozo wa Roho Mtakatifu 
Yupo Morogoro Veta Dakawa 

Walengwa ni walioahidiwa Ahadi na Bwana hazijatimizwa mpaka Leo.

Nakukakaribisha Soma kwa rudia rudia uelewe vyema.

TUEPUKE HAYA ILI KUMFANYA ATIMIZE ALIYOTUAHIDIA.
1:TUSIACHE KUTII ANGIZO LAKE.

2:TUSIMUASI MUNGU TUKARUDIA DHAMBI TULIZOZIACHA.


MAMBO AMBAYO YAFANYE KUFIKIA AHADI YA MUNGU.

1:UWE NA MOYO WA TOBA.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mungu anapeΓ±da uwe mwepesi wa kutambua hili namkosea Mungu hili niko sahihi kisha umrundie yeye kwa maombi ya machozi jutia na umia kukosana na Mungu. 

2 Mambo ya Nyakati 7:14
[14]ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 

2.UTII NA KUFATA MAELEKEZO AKUANGIZAYO MCHUNGAJI. 

Jifunze kutii na kufata maangizo unayopewa na mchungaji maana ndani yake lipo Neno la Mungu Ambalo Mungu ameliweka ndani ya kinywa chake mtumishi. 

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Kumbukumbu la Torati 28:1
[1]Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 

3:MUITE MUNGU KWA KUOMBA.

Jifunze kuomba usitake Mungu kumwambia atende kitu kwako wakati wewe humuiti Baba Yako wa Mbiguni. Kuna vitu huvijui unatakiwa uombe Mungu akufunulie yanayokutesa.

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Yeremia 33:3
[3]Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. 


4.SAMEHE WATU MAKOSA YAO.

Mungu anaweza akawa amenyamaza Asikujibu kwa sababu umebebelea watu moyoni mwako Hutaki kuwatua achilia ufunguliwe. Neno linasema hivi
Kusamehe ni kitendo cha kufuta na kusahau kabisa ulichowahi kutendewa.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mathayo 6:14
[14]Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 

HAYA YAPITIE UHAKIKISHE UMEYATIMIZA NA BADO UNAONA AHADI ZAKE MUNGU KWAKO BADO.

OMBA HIVI MKUMBUSHE.

1;Umesema Utayatimiza mapenzi yako sawasawa na ahadi zako kwangu Bwana tazama nimekuwa mwaminifu kwako kwa kila unachoniangiza kupitia mtumishi wako Pastor Richard Nasimamia mstari huu nikumbushe kwako
Isaya 55:11
[11]ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. 

Tamka huu mstari kisha malizia katika Jina la Yesu.Amen 




2.Bwana Umesema Mke mwema au mume mwema niwewe umjuaye mimi simjui nataka uniletee muda wangu umefika wa kuwa na mtu uliyemwandaa kwa ajili yangu nasimama na mstari huu kukumbusha nao  unasema
Mithali 31:10
[10]Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? 
Maana kima chake chapita kima cha marijani. 

Tamka kwa kusoma huu mstari malizia katika jina la Yesu. Amen


3.Bwana nipo napitia mateso napitia mahagaiko ya hii dunia mpaka nafikia hatua nasema Mungu wangu umeniacha nakumbuka Neno lako la Maombolezo linanipa tumaini jipya umesema hupendi niteseke kwanini Bwana unaniangalia tu nateseka mwanao Dhibitisha Neno lako hili

Maombolezo 3:33
[33]Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. 
Wala kuwahuzunisha. 

Malizia kwa kutamka huu mstari .

4.Nashukuru Kwa Yote Bwana Bado utabaki kuitwa Mungu kwangu haijalishi nipitie nyakati ngani vipindi ngani Bado wewe ni Mungu nifundishe nijue kusema Nashukuru maana ndilo Neno nzuri umesema kuliko yote 
Zaburi 92:1
[1]Ni neno jema kumshukuru BWANA, 
Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. 


Endelea Kusema na Mungu kwa kuweka mstari aliosema kwako na bado hajatenda lakini hakikisha umepitia toba na umesamehe na unatii maangizo ya Bwana.


Na Ubarikiwe uliyeweza kujifunza kitu na umeongeza ufahamu 


Unaweza shirikisha wegine

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.