SOMO:FIKIRI KABLA YA KULALAMIKA

SOMO:FIKIRI KABLA YA KULALAMIKA MUNGU HAKUJIBU.

Kuna maandiko Ambayo yanakupa picha na mwelekeo katika maisha yako ya wokovu ni vyema ukayajua nakuyashika Kabla hujaanza kutupia lawama Mungu hakujibu hakusikii.

Wapo wegine wanawaza kufa wegine waache kanisani kisa Mungu hatendi
Kumbe matatizo mengine shida ipo kwako unaona yaleyale hutaki kuona ushindi
Muulize batrimayo kipofu alibadili mtazamo akaanza kuona ushindi mafanikio  kustawi
Nawewe fikira zako ziponywe kwa jina la Yesu.

Nakukaribisha katika Somo hili ninayekuandalia Pastor Richard kwa msaanda wa Roho Mtakatifu. 
Nipo Morogoro Kanisa la H.S.C.T

1;JAMBO LA KWANZA MPENDE MUNGU KWA AKILI  ZAKO ZOTE NAFSI YAKO ZOTE.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mathayo 22:37
[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 
 
Vipimo vya Kumpenda Mungu Kweli.

1.Uvumilivu wako katika nyakati zote anapochelewa kujibu.

2.Kujitoa Kwako kwa Kazi ya Mungu katika Sadaka zako Viwanja magari na nyumba.

Ufahamu na uelewa mkubwa wa Kumtolea Mungu kuliko kusubiri kupikea .


3.Imani yako kuamini kila kitu Kinawezekana Nakuanza kuona umevuka kabla ya kuvuka.

4.Muda wako wa ibada na Mungu kutoa Muda ufanye ibada na Mungu.

5.Kuchukia dhambi nakutafuta maisha matakatifu. Na Kutokukubalu kumaliza mwendo wa hapa duniani hujaacha alama kwa Bwana 
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Huwezi Sema Unampenda Mungu imani yako haina imani ya utoaji imani ya kubadilika imani ya kuona ushindi


2.USIZINI.
Tusome huu mstari
Mathayo 5:27
[27]Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 

Kwanini Yesu Anaanza Kwa Kutuuliza Kwa Sababu Wapo watu wanajua kabisa kuzini ni dhambi  lakini wanazini na wanasingizia tamaa zao na hisia zao wanashindwa kuzizuia Yesu akasema Basi acha kutamani maana hata ukitamani mawazo yanakupeleka kuzini umekosa tayari.

Kuzini ni Kufanya tendo la ndoa mtu ambaye hujamtolea mahari  wazazi hawajakukabidhi Tayari unaitwa unazini hii huwa lango kubwa la wewe kuteswa kwenye uchumi mahusiano na kudharaulika katika Jamii. 

UNAPOAMBIWA USIZINI NA NENO maaana yake ni Amri hiyo umepewa.


3:USI- SITE  KATIKA MAAMUZI YAKO.

Kama umeamua kubadilika kumfa Mungu mfate Mungu Kama Umeamua Kufata Dunia Ifate Dunia.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡Mungu anawachukia watu wakusitaπŸ‘‡πŸ‘‡
Zaburi 119:113
[113]Watu wa kusita-sita nawachukia, 

Hata Elia aliwaambia watu mtasi sita mpaka lini kwa maana michanganyo mnaitaka na Mungu mnamtaka chagueni Leo.

Maisha yako yanaitaji ufanye uchanguzi sahihi sasa hivi usielemewe na mawazo mawili ambayo kesho yatasababisha uende motoni kwa kuwa imani uliondoa ukaweka kusitasita ni hatari sana 

Soma mstari huu
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
1 Wafalme 18:21
[21]Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno. 

4:TOA KWA AJILI YA BWANA.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Matendo:5 Matendo :10

Inaongelea mtu aliyekuwa mtoaji kwa Mungu na mtu aliyekuwa anatoa lakini kwa kumwimbia Mungu.

Wewe usimwimbie Bwana toa kikamilifu uone Mungu anavyoenda kushughulika nawewe.

Matendo ya Mitume 10:4
[4]Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. 

Maombi yako unaweza ukawa unaomba hayafiki kwa Mungu sababu hutoagi huna alama yenye ukumbosho kwa Mungu. Jifunze kutoa kwa Mungu.

5:USIKATE TAMAA

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mhubiri 2:20
[20]Kwa hiyo nikageuka kukata tamaa moyoni mwangu juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua. 

Unapokata tamaa ni kukubali kuwa Mungu uliyembeba  Amezidiwa hawezi kukusaindia au Kukuvusha wewe katika changamoto yako.

Lakini Kama Mungu wako ukimwelewa vizuri hutaka tamaa katika mashindano ya hapa Duniani. 

.6:USIOMBE UKIWA NA UCHUNGU.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Ayubu 21:25
[25]Mwingine hufa katika uchungu wa roho, 
Asionje mema kamwe. 


Mtu mwenye uchungu humzuia Mungu asimjibu kutokana na Uchungu alionao.

Wapo watu maombi yao hayajibiwi kutokana na Uchungu walio nao moyoni.


TUFANYE NINI SASA.

Tufikirie Kabla hatujaanza kulalamika ninaomba ninafunga fungu lakumi natoa.
Jiulize haya.
 Je,huzini Je, husiti husiti Je, hujakata tamaa 


Tengeneza Na Mungu Sasa Uone Mungu atakavyobadili maisha yako.

Unapoomba Amini moyonu mwako kwenye akili zako kuwa Mungu Ametenda Anza Kuona Upo ndani ya Shera anza Kuona wewe mwaka huuu unapakata watoto 6 yaana mapacha sita Anza kuona cheo chako kinapanda one sasa visa ya kwenda ulaya unaenda kuichukua badili fikira zako usione mateso usione Upofu one unamacho wewe na unaona unaona Usiseme wewe masikini au wewe wa mahagaiko kataa hiyo hali.

Imani ipo kwako wewe kuona ushindi katikati ya ule udhaifu ulionao .


Mwisho 

SHUKURANI ZANGU KWENU.

Ansateni Wote Wanangu mnaoendelea kushiriki kwa kujitoa pesa zenu mali zenu viwanja vyenu kwa ajili ya kazi hii ya Mungu.

Kama Ambavyo nilisema Taasisi hii ya kidini inaitwa Holy Spirit church Tanzania  imeanzishwa na Pastor Richard  Haina mfadhili au haina inajiendesha yenyewe Na nyie watoto wangu mumekuwa mkihakikisha kazi Ya Mungu inasonga mbele wengine kutoa viwanja kwa ajili ya ujezi wa makanisa.

Nawaombea wote mnaojitoa kwa kazi hii ya Mungu azidi kuwaonekania sababu mwafanya vitu vikubwa mno hata mnaokesha mkiombea.

Tuma maoni yako kuhusu chochote unachoshuhudiwa kwa ajili ya Taasisi hii WhatsApp 
+255759861768

Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.