SOMO; MAVAZI NI UTAMBULISHO WAKO ULIYAVAA.

SOMO: MAVAZI NI UTAMBULISHO WAKO WEWE ULIYEYAVAA.

Nakukaribisha katika Somo hili;
Mavazi unaweza Kuvaa wewe mwenyewe unavyotaka Jamii ikutambue au Mbigu zikuelewe. Mavazi ni uhuru wa mtu kuvaa anavyoona nafsi yake yafaa.

Lakini tambua Kila Vazi ukilivaa Tunajua huyu ni nani.
Mfano ukivaa Joho na kofia tunajua huyu mhitimu amesoma Ukivaa Sale za kazini kwako tunatambua kupita mavazi uliyovaa.
Nakukaribisha upate kuongeza maarifa

KUNA AINA NNE NIMEPATA KATIKA UVAAJI

1:UVAAJI WENYE UTUKUFU

Haya ni mavazi yanayompa utukufu Mungu yenye heshima yaliyoshonwa vyema na kwa kitabaa safi isiyoonesha maungo yako ya ndani
Soma 👉Luka;7;25 Kutoka:31:10 
Walawi:16;32

2:UVAAJI WA KITUMWA.

Haya ni mavazi yanayomtambulisha mtu anatumikishwa na kitu au amefungwa mfano.
Chizi, mtu aliyefungwa uvaaji wake utajua tu.

Ukija kuvaa mavazi hayo wewe ambaye siyo tayari jamii na watu tutambua umetekwa na roho wewe unatumikia kifungo fulani.

TUSOME ANDIKO. Kumb.Torati:21:13


3.UVAAJI WA KIKAHABA

Kahaba ni mwanamke mwenye zaidi ya waume wawili anaweza akawa hajipangi kujiuza mwili wake lakini anatabia ya kubadili wanaume hana msimamo na mtu mmoja.

Uvaaji wake na anavyojiweka mwenyewe Jamii humtambua na kumjua kuwa huyu ni kahaba moja ya utambulisho wake ni uvaaji wake. Anavaa nguo fupi zenye kuonyesha mwili wake kwa ajili ya kuvutia wateja wake.

Tusome  Mithali;7;10

Wewe ambaye huna Tabia hiyo Jamii ikikuona umevaa mavazi hayo itakutambua kama kahaba  hata wanaume watakaovutiwa kuja ni wenye kuzini nawewe siyo kukuowa.



4;UVAAJI WA KIFALME. 

Tusome. Esta:6;8 Matendo:12;21 Esta.8:15

Haya ni mavazi ya kiutawala mfano Jeshi, Rais ,Mfalme ,mchungaji ,Doktari, Nesi, Nk

Mavazi hayo ukivaa utakuwa na nguvu ya kusikilizwa kutoa msaada na kukusanya watu.

Mfano. Wewe siyo Police uvae mavazi ya Kipolice au wewe siyo mwanajeshi uvae vazi la kijeshi Utakamatwa na kuadhibiwa sababu unajaribu kuutambulisha Jamii wewe ni mtu fulani kumbe Siyo.

Kutokana mavazi ya kiutawala ukiyavaa lazima nawe uwe mtawala katika eneo hilo.

Kama mtoto wa Mungu uliyeokoka ni vyema uvae vazi lenye heshima linalokutambulisha wewe kweli umeokoka na umebemba Jina lenye nguvu Ambalo ni Yesu.



Vaa vizuri nyosha nguo zako vizuri jiweke Simant ili hata Ambao utaenda kuwapasha habari njema za Yesu Wasadiki kweli.


MWISHO 

Kila uvaaji unaopenda kuuvaa unakutambulisha katika Jamii wewe ni nani utambulisho wa kwanza katika ulimwengu wa roho na mwili ni uvaaji wako.

Kwa hiyo upo huru kuvaa utakavyo kuligana na nafasi ya uvaaji wa haya makundi niliyoyataja.

Wewe unapenda kuvaa mavazi yapi na Jamii I akitembea hivyo unavyovaaga au.


Basi somo hili unaweza kushare kama limekubariki 

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.